انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣٣

قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُۥ لَيَحْزُنُكَ ٱلَّذِى يَقُولُونَ ۖ فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ ٱلظَّـٰلِمِينَ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ يَجْحَدُونَ ٣٣

{33} Yaani, hakika tunajua ya kwamba hayo wanayoyasema wale wanaokadhibisha kukuhusu yanakuhuzunisha na yanakuwiya mabaya. Na hatukukuamrisha yale tuliyokuamrisha ya kuwa na subira isipokuwa tu ili upate vyeo vya juu na hali za thamani. Kwa hivyo usifikiri kwamba kauli yao hiyo inatokana na kuwepo mchanganyiko katika jambo lako na hata kukuhusu wewe mwenyewe. "Hakika wao hawakukadhibishi wewe" kwa sababu wao hakika wanajua ukweli wako, na kuingia kwako na kutoka kwako, na hali zako zote; kiasi kwamba kabla ya utume wake walikuwa wakimuita Al-Amin. "Lakini hao madhalimu wanazikataa ishara za Mwenyezi Mungu," yaani, kukadhibisha kwao huko ni kukadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu alizoweka Mwenyezi Mungu juu ya mikono yako.