انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٣

هُوَ ٱلَّذِى يُرِيكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ وَيُنَزِّلُ لَكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ رِزْقًا ۚ وَمَا يَتَذَكَّرُ إِلَّا مَن يُنِيبُ ١٣

{13} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja neema zake kubwa juu ya waja wake kwamba aliwabainishia haki mbali na batili kupitia yale anayowaonyesha waja wake ya aya zake za kinafsi, za kwenye upeo wa macho na za katika Qur-ani zinazoashiria kila linalotafuta na lililokusudiwa, na zinazobainisha uongofu kutokana na upotofu, kiasi kwamba mwenye kuziangalia na kuzitafakari hawezi kubaki na shaka hata kidogo katika kujua uhakika. Hii ni katika neema zake kubwa juu ya waja wake, kwani hakuiacha haki ikiwa na mchanganyiko na wala hakuliwacha jambo lililo sahihi kuwa na utata wowote. Bali aliweka aina mbalimbali za ishara na akazibainisha Aya mbalimbali ili mwenye kuangamia aangamie kwa hoja zilizowazi, na aishi atakayeishi kwa hoja zilizowazi. Na kila masuala yanavyokuwa matukufu na makubwa zaidi, ushahidi wake unakuwa mwingi na mwepesi zaidi. Hebu tazama suala la upweke wa Mwenyezi Mungu, kwa maana ndilo suala kubwa zaidi, zilikuja hoja nyingi sana juu yake, za kiakili na za kimaandiko, na Mwenyezi Mungu akazipigia mifano na hoja mbalimbali. Basi ndiyo maana akataja na kuashiria mahali hapa baadhi ya ushahidi wake. Alisema: "Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu." Na alipotaja kuwa Yeye huwaonyesha waja wake Ishara zake, akatanabahisha juu ya ishara kubwa, akasema: "Na anakuteremshieni kutoka mbinguni riziki." Yaani, mvua ambayo kwayo mnapata riziki nyinyi na mifugo wenu na mnaishi kwayo. Hilo linaashiria kwamba neema zote zinatoka kwake. Miongoni mwake ni neema za kidini, ambazo ni masuala ya kidini na ushahidi wake, na kufanya matendo mema yanayoufuata ushahidi huo. Na pia kuna neema zote za kidunia kama vile neema zinazotokana na mvua, ambayo kwayo nchi na watu wanakuwa hai. Hili linaonyesha kwa njia ya uhakika kwamba Yeye peke yake ndiye afaaye kuabudiwa, ambaye anafaa kukusudiwa peke yake katika dini, kama vile Yeye peke yake ndiye anayeneemesha. "Na hapana anayekumbuka" kwa ishara hizi anapokumbushwa "ila anayerejea" kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumpenda, kumnyenyekea na kumtii. Huyu ndiye anayenufaika kwa ishara hizo, nazo zinakuwa ni rehema kwake, na kwazo anazidi kuwa na ufahamu mkubwa.