انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٤

فَٱدْعُوا۟ ٱللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْكَـٰفِرُونَ ١٤

{14} Na kwa kuwa ishara zinaleta ukumbusho, na kukumbuka kunalazimu kwamba mja amkusudie Mwenyezi Mungu peke yake, akasema: "Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu." Hili linajumuisha kumuomba kwa kumfanyia ibada na kumuomba dua. Ikhlasi inamaanisha kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika ibada zote za faradhi na zinazopendekezwa katika haki za Mwenyezi Mungu na katika haki za waja wake, "hata kama makafiri watachukia." Basi msiwajali, na wala hayo yasikuzuieni mbali na Dini yenu, wala msiijali lawama ya mwenye kuwalaumu kwa sababu ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana, makafiri wanachukia suala la kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake kwa chuki kubwa sana. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake, nyoyo za wale wasioiamini Akhera huchafuka. Na wanapotajwa wenginewe wasiokuwa Yeye, basi wao hufurahi."