غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ذَٰلِكُم بِأَنَّهُۥٓ إِذَا دُعِىَ ٱللَّهُ وَحْدَهُۥ كَفَرْتُمْ ۖ وَإِن يُشْرَكْ بِهِۦ تُؤْمِنُوا۟ ۚ فَٱلْحُكْمُ لِلَّهِ ٱلْعَلِىِّ ٱلْكَبِيرِ ١٢
{12} Walikemewa kwa kutofanya visababu vya wokovu, basi wakaambiwa: "Hayo ni hivyo kwa sababu mlikuwa akiombwa Mwenyezi Mungu peke yake" ili apwekeshwe na akusudiwe Yeye tu na kutomshirikisha, "mnamkufuru." Na nyoyo zenu zimechukizwa kwa hayo, na mnajitenga nayo kujitenga kukubwa. "Na akishirikishwa, mnaamini." Haya ndiyo yaliwafikisha mahala hapa, kwani mlikuwa mkikufuru Imani na mnaamini ukafiri. Mkawa mnaridhia maovu na uharibifu duniani na Akhera, na mnachukia mema na ya kuwafanya mtengenee katika dunia na Akhera. Mlikuwa mkipendelea sababu za kujitia mashakani, katika fedheha na ghadhabu, na mnakata tamaa ya kufikia yale ambayo ni sababu ya kufaulu na kushinda. "Wakiiona njia ya uwongofu, hawaishiki kuwa ndiyo njia lakini wakiiona njia ya upotofu, wanaishika kuwa ndiyo njia." "Basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Mkuu." Ni Mtukufu kwa namna zote: kwa dhati yake, cheo na ushindi. Na katika utukufu wa cheo chake ni ukamilifu wa uadilifu wake, na kwamba Yeye huweka vitu mahali pake, na wala hatoshanishi watu wema na waovu. Naye ni Mkubwa ambaye anao ukubwa wote, ukuu na utukufu katika majina yake, sifa zake na vitendo vyake, aliyetakasika mbali na kila kasoro na upungufu. Kwa hivyo, ikiwa hukumu ni yake, na tayari alishawahukumia kwamba mtaishi milele daima, basi hukumu yake haitageuka wala haitabadilika.