انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢٥

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَٱتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَٰهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَٱتَّخَذَ ٱللَّهُ إِبْرَٰهِيمَ خَلِيلًا ١٢٥

{125} Yani Hakuna aliye bora zaidi katika dini kuliko mwenye kujumuisha kati ya ikhlasi kwa mwabudiwa wake, ambayo ni kuusalimisha uso kwa Mwenyezi Mungu, kwenye kuashiria kujisalimisha kwa moyo, na kuelekea kwake, na kurudi kwake, na ikhlasi yake, na kuelekea uso na viungo vyote kwa Mwenyezi Mungu. "Hali ya kuwa yeye" pamoja na ikhlasi hii na kujisalimisha "ni mwema." Yaani mwenye kufuata sheria ya Mwenyezi Mungu ambayo Mwenyezi Mungu aliwatuma kwayo Mitume wake, na akateremsha Vitabu vyake, na akaifanya kuwa ni njia ya wateule katika viumbe wake na wafuasi wao, "na akafuata mila ya Ibrahim mnyoofu." Yani Dini yake na sheria yake "mnyoofu." Yani aliyejiepusha na ushirikina na akaielekea Tauhidi, na kuacha kuwaelekea viumbe na akamuelekea Muumba. "Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwandani." Na urafiki mwandani ndio upendo wa hali ya juu kabisa. Na daraja hii iliwatokea marafiki wandani wawili wa Mwenyezi Mungu: Muhammad na Ibrahim baraka na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao. Ama upendo utokao kwa Mwenyezi Mungu, basi huo ni kwa Waumini wote, lakini Mwenyezi Mungu alimchukua Ibrahimu kama rafiki mwandani kwa sababu alitimiza yale aliyoamrishwa, na akafanya yale aliyojaribiwa kwayo. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamfanya kuwa imamu wa watu, na akamchukua kuwa rafiki mwandani, na akauinua utajo wake katika walimwengu.