النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَن يَعْمَلْ مِنَ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ يَدْخُلُونَ ٱلْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ نَقِيرًا ١٢٤
{124} "Na mwenye kufanya katika mema," yaliingia katika hilo matendo mengine yote ya kimoyo na ya kimwili, na yaliingia pia kila mtenda matendo miongoni mwa binadamu au jini, mdogo au mzee, wa kiume au wa kike. Ndiyo maana akasema, “akiwa wa kiume au wa kike, naye ni Muumini.” Na hili ni sharti la matendo yote, hayawi mema, wala hayakubaliwi wala hayaambatani nayo malipo, wala haizuiliki kwayo adhabu isipokuwa kwa imani. Kwa hivyo matendo pasipo imani ni kama matawi ya mti ambao mizizi yake imekatwa, na ni kama jengo lililojengwa juu ya mawimbi ya maji. Basi Imani ndio asili, na asasi, na msingi ambao kila kitu kinajengwa juu yake. Na kizuizi hiki ni lazima kizingatiwe katika kila tendo lolote lile. Kwa kuwa hilo ndilo tendo limefungwa kwacho. "Basi hao;" yani, wale waliojumuisha kati ya Imani na matendo mema "wataingia Peponi." Inajumuisha yale yanayotamaniwa na nafsi na macho yanafurahia; "wala hawatadhulumiwa kiasi cha jicho la kokwa ya tende." Yani, si kidogo wala kingi katika yale waliyoyafanya ya heri, bali watayakuta yakiwa kamili, mengi, yamezidishwa mizidisho mingi.