الزمر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ تَرَى ٱلَّذِينَ كَذَبُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ وُجُوهُهُم مُّسْوَدَّةٌ ۚ أَلَيْسَ فِى جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْمُتَكَبِّرِينَ ٦٠
{60} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaeleza juu ya fedheha ya "wale waliomsingizia uongo Mwenyezi Mungu " na kwamba nyuso zao Siku ya Kiyama "zitakuwa nyeusi" kana kwamba ni usiku totoro. Hivyo ndivyo watakavyowajua watu watakaokuwa hapo siku hiyo. Kwani, haki ni wazi kabisa kana kwamba ni asubuhi. Kama vile walivyofanya uso wa haki kuwa mweusi kwa uongo wao; Mwenyezi Mungu akazifanya nyuso zao kuwa nyeusi kama malipo ya aina sawa na matendo yao. Kwa hivyo, watakuwa na nyuso nyeusi, na watapata adhabu kali katika Jahannamu. Ndiyo maana akasema: "Je, si katika Jahannamu makazi ya wanaotakabari," wakaikataa haki na wakakataa kumuabudu Mola wao Mlezi, na wakamzulia uongo? Ndiyo, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu. Ndani yake kuna adhabu, fedheha na ghadhabu itakayowafikia wafanyao kiburi hao kila kiwango, na haki yote itachukuliwa kutoka kwao. Kusema uwongo juu ya Mwenyezi Mungu kunajumuisha kumfanyia mshirika, mtoto, mke, kusema juu yake mambo yasiyoufailia utukufu wake, au kudai unabii, au kusema katika sheria yake kitu ambacho hakukisema na kusema kuwa alikisema na akakiweka katika sheria.