انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الزمر
السورة ٣٩

الزمر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦١

وَيُنَجِّى ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ بِمَفَازَتِهِمْ لَا يَمَسُّهُمُ ٱلسُّوٓءُ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ٦١

{61} Alipotaja hali ya wenye kiburi, akataja hali ya wachamungu, akasema: "Na Mwenyezi Mungu atawaokoa wenye kujikinga kwa ajili ya kufuzu kwao," na hilo ni kwa sababu wanacho chombo cha kuokoka ambacho ni ucha Mungu, ambao ndiyo maandalizi bora zaidi wakati wa kila hofu na dhiki. "Hapana uovu utakaowagusa" ukawawia vibaya, "wala hawatahuzunika." Hapa akasema kwamba hakuna adhabu na hofu yake itakayowasibu, na hiyo ndiyo amani ya juu kabisa, ambayo itaandamana nao mpaka iwafikishe katika nyumba ya salama. Hapo, watakuwa na amani kutokana na kila ubaya na machukizo, na watakuwa na mng'aro wa neema, watasema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetuondolea huzuni zote. Hakika Mola wetu Mlezi bila ya shaka ni Mwenye kusamehe, Mwenye shukrani sana.