انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨

عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يَرْحَمَكُمْ ۚ وَإِنْ عُدتُّمْ عُدْنَا ۘ وَجَعَلْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَـٰفِرِينَ حَصِيرًا ٨

{8}"Huenda Mola wenu Mlezi akawarehemu." Kwa hivyo aliwarudishia zamu dhidi yao. Basi akawarehemu na akawarudishia zamu lakini akawatishia kwamba wasiasi. Akasema, "na mkirudia" katika kufanya uharibifu katika ardhi, "tutarudia" kuwaadhibu. Kwa hivyo, wakalirudia hilo. Basi Mwenyezi Mungu akampa mamlaka Mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - dhidi yao na Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa yeye. Haya ndiyo malipo ya duniani. Na ama adhabu iliyo mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa na mbaya zaidi. Na kwa sababu hii akasema, "Na tumeifanya Jahannam kuwa ni gereza kwa ajili ya makafiri." Wataingia na kukaa humo na hawatatoka humo kamwe. Katika aya hizi, kuna onyo kwa umma huu juu ya kufanya maasia, ili wasipatwe na yale yaliyowapata Wana wa Israili. Kwa maana, desturi ya Mwenyezi Mungu ni moja, haibadiliki wala haigeuki. Na mwenye kutazama namna makafiri na madhalimu wamepewa mamlaka juu ya Waislamu, atatambua kuwa yote hayo ni kwa sababu ya madhambi yao, na hilo ni ili iwe ni adhabu kwao. Na kwamba wakisimamisha Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume wake, atawaimarisha katika ardhi na atawasaidia dhidi ya maadui zao.