انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٩–١٠

إِنَّ هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانَ يَهْدِى لِلَّتِى هِىَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ ٱلْمُؤْمِنِينَ ٱلَّذِينَ يَعْمَلُونَ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا ٩ وَأَنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ١٠

{9-10} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya heshima na utukufu wa Qur-ani na kwamba, "inaongoa kwenye yale yaliyonyooka kabisa." Yaani, maadilifu zaidi na ya juu zaidi miongoni mwa itikadi, matendo na tabia. Kwa hivyo yeyote atayeongoka kwa kile ambacho Qur-ani inalingania, anakuwa mkamilifu zaidi wa watu, na mnyoofu zaidi, na mwongofu zaidi katika mambo yote. "Na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema" miongoni mwa mambo ya wajibu na mambo yapendekezwayo, na "ya kwamba wana malipo makubwa;" ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia katika nyumba ya utukufu wake ambayo hajui maelezo yake na sifa zake isipokuwa yeye tu. "Na ya kwamba wale wasioiamini Akhera tumewaandalia adhabu chungu." Kwa maana Qur-ani ndani yake kuna bishara na maonyo. Na imetaja sababu ambazo bishara hupatikana kwazo, ambazo ni imani na matendo mema, na mambo ambayo kwayo anastahiki onyo, nayo ni kinyume cha hayo.