الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنْ أَحْسَنتُمْ أَحْسَنتُمْ لِأَنفُسِكُمْ ۖ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا ۚ فَإِذَا جَآءَ وَعْدُ ٱلْـَٔاخِرَةِ لِيَسُـۥٓـُٔوا۟ وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا۟ ٱلْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا۟ مَا عَلَوْا۟ تَتْبِيرًا ٧
{7} "Mkifanya wema mnafanyia wema nafsi zenu." Kwa maana faida yake itawarudia nyinyi wenyewe hata katika dunia hii, kama mlivyoona kutokana na ushindi wenu juu ya maadui zenu. "Na mkifanya ubaya, basi mnajifanyia wenyewe." Yaani, madhara yake yanawarudia nyinyi wenyewe, kama vile Mwenyezi Mungu alivyowaonyesha kwa kuwapa mamlaka maadui. "Na ikifika ahadi ya mwisho;" yaani, mara ya pili mtakapofanya uharibifu katika ardhi, tutawapa mamlaka maadui dhidi yenu tena, "ili waziharibu nyuso zenu" kwa kuwashinda nyinyi na kuwateka. "Na waingie msikitini kama walivyoingia mara ya kwanza." Makusudio ya msikiti hapa ni msikiti wa Bayt Al-Maqdis. "Na waharibu;" yaani, kubomoa na kuharibu "kile walichokiteka, kwa uharibifu mkubwa" kwa kubomoa nyumba zenu, misikiti yenu, na mashamba yenu.