الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَن كَانَ فِى هَـٰذِهِۦٓ أَعْمَىٰ فَهُوَ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ أَعْمَىٰ وَأَضَلُّ سَبِيلًا ٧٢
{72} "Na yule ambaye ni kipofu hapa" duniani asiijue na kuikubali haki, wala kuifuata, bali alifuata upotofu, "basi atakuwa kipofu Akhera" asiweze kushika njia ya peponi kwa vile hakuishika duniani, "na atakuwa ndiye mpotovu zaidi wa Njia." Kwa kuwa malipo ni kwa aina sawa na matendo. Na kama unavyotenda, ndivyo utakavyotendewa. Na katika Aya hii, kuna ushahidi kwamba kila umma utaitwa kwenye dini yake na kitabu chake. Na je, ulitenda kwa kufuata hayo au la? Na kwamba hawataadhibiwa kwa sheria ya Nabii ambaye hawakuamrishwa kuifuata, na kwamba Mwenyezi Mungu hamuadhibu yeyote isipokuwa baada ya kusimama hoja juu yake naye akaihalifu. Na kwamba watu wema watapewa vitabu vyao kwa mikono yao ya kulia, na watapata furaha nyingi, na kwamba watu waovu wako kinyume na hayo, na kwamba hawataweza kusoma vitabu vyao kwa sababu ya ukubwa wa dhiki yao, na huzuni yao, na kuangamia kwao.