الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِن كَادُوا۟ لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ ٱلَّذِىٓ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ لِتَفْتَرِىَ عَلَيْنَا غَيْرَهُۥ ۖ وَإِذًا لَّٱتَّخَذُوكَ خَلِيلًا ٧٣
{73} Yeye Mtukufu anataja neema yake kwa Mtume wake Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na kumhifadhi kwake kutokana na maadui zake ambao walikuwa na bidii ya kumjaribu kwa kila njia. Akasema, "Na hakika walikaribia kukushawishi uache hayo tuliyokufunulia ili utuzulie mengineyo." Yaani, walikupangia jambo baya ambalo hawakufanikiwa kulifikia, na wakakuhadaa ili umzulie Mwenyezi Mungu mambo ambayo hakukuteremshia, ili useme yale yanayoafikiana na matamanio yao, na uyaache yale aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu. "Na hapo" lau ungefanya yale wanayotamani, "ndipo wangelikufanya mwandani" na kipenzi zaidi kwao kuliko wapenzi wao, kwa sababu ya maadili mema na tabia njema alizokuumba nazo Mwenyezi Mungu, ambazo zinamvutia walio karibu na walio mbali, rafiki na adui. Lakini ujue ya kwamba hawakukufanyia uadui na kukukanusha kwa uadui, isipokuwa kwa sababu ya haki ambayo ulikuja nayo, si kwa ajili yako mwenyewe, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Hakika tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha hayo wanayoyasema. Basi hakika wao hawakukadhibishi wewe, lakini hao madhalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu."