انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧١

يَوْمَ نَدْعُوا۟ كُلَّ أُنَاسٍۭ بِإِمَـٰمِهِمْ ۖ فَمَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ يَقْرَءُونَ كِتَـٰبَهُمْ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا ٧١

{71} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu hali ya viumbe Siku ya Qiyama, na kwamba atawaita kila kikundi cha watu pamoja na imamu wao na mwongozi wao kwenye njia iliyonyooka, na wao ni Mitume na wawakilishi wao. Kwa hivyo kila umma watahudhurishwa, na atakuwepo Mtume wao aliyewalingania, na matendo yao yatawasilishwa mbele ya Kitabu alicholingania Mtume wao, je yanaafikiana nacho au hapana? Kisha watagawanyika katika makundi mawili, "basi atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia," kwa sababu alimfuata imamu wake, kiongozi kwenye njia iliyonyooka, na akaongoka kwa kitabu chake, basi mazuri yake yakakithiri, na maovu yake yakawa machache. "Basi hao watasoma kitabu chao" kisomo cha furaha na uzuri kwa sababu ya yale wanayoyaona humo, katika yale yenye kuwafurahisha, "wala hawatadhulumiwa hata chembe."