انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٠

وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِىٓ ءَادَمَ وَحَمَلْنَـٰهُمْ فِى ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ وَرَزَقْنَـٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ وَفَضَّلْنَـٰهُمْ عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا ٧٠

{70} Na hili ni katika ukarimu wake kwao na wema wake, ambao thamani yake haina kipimo. Ambapo aliwatukuza wanadamu kwa kila njia za kutukuza. Basi akawatukuza kwa elimu na akili, na kuwatuma Mitume, na kuwateremshia vitabu, na akawafanya vipenzi vyake miongoni mwake, na wateule, na akawaneemesha kwa neema zilizo wazi na zilizofichika. "Na tukawabeba katika nchi kavu" juu ya vipando kama vile ngamia, nyumbu, na punda, na vipando vinginevyo vya nchi kavu. Na "baharini" katika majahazi na meli "na tukawaruzuku katika vitu vizuri vizuri" kama vile vyakula, vinywaji, nguo, na mambo ya ndoa. Basi hakuna chochote kizuri kinachohusiana na mahitaji yao isipokuwa Mwenyezi Mungu amewatukuza kwacho na amewarahishia hilo kabisa "na tukawafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa wale tuliowaumba," kwa mambo maalumu aliyowapa kama vile sifa nzuri, na akawafadhilisha kwazo kwa namna ambayo hakuna wengine walizo nazo miongoni mwa aina mbalimbali za viumbe. Je, basi hawatamshukuru aliyewafikishia neema hizi na akawazuilia maangamivu? Na wala zisiwazuie neema hizo dhidi ya aliyezineemesha kwa hivyo zikawashughulisha wasimuabudu Mola wao Mlezi. Bali huenda wakazitumia neema kuwasaidia katika kumuasi.