الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
سُبْحَـٰنَهُۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يَقُولُونَ عُلُوًّا كَبِيرًا ٤٣
{43} "Subhanahu Wa Taa'la (Ametakasika na Ametukuka juu kabisa) na sifa zake ziko juu zaidi "na hayo wanayoyasema," kwamba ana mshirika, na kumfanyia wenza pamoja naye. Yeye hadhi yake iko juu sana, na ukubwa wake ni mkuu, na mtukufu zaidi kiasi kwamba haiwezekani kuwepo na miungu pamoja naye. Kwa hivyo amekwisha potea mwenye kusema hivyo upotevu ulio wazi na akadhulumu dhuluma kubwa. Kwa maana, viumbe vyote vikubwa ni duni mbele ya ukuu wake, ni hata mbingu saba na vilivyo ndani yake na ardhi saba na vilivyo ndani yake ni vidogo mno mbele ya ukubwa wake. Na Siku ya Qiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume. Na ulimwengu wa juu na wa chini unamhitaji uhitaji wa kidhati ambao hauachani na yeyote kati yao wakati wowote ule. Nako ni kuhitaji kwa aina zake zote. Kuhitaji katika upande wa kuumbwa, kuruzukiwa, na kuendeshwa. Na kuhitaji katika upande wa ulazima ulioko kwamba awe yeye ndiye Muabudiwa wao, na Mpendwa wao ambaye wanajiweka karibu naye, na ambaye wanamkimbilia katika kila hali.