انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٤

تُسَبِّحُ لَهُ ٱلسَّمَـٰوَٰتُ ٱلسَّبْعُ وَٱلْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَىْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِۦ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ٤٤

{44} Na ndiyo sababu akasema, "Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake ijapokuwa hakuna kitu" miongoni mwa wanyama anayezungumza na asiyezungumza, na miti, mimea na vyote visivyo hai na vilivyo hai, na wafu, "ila kinamtakasa kwa sifa zake," kwa hali zao mbali mbali na hata kwa maneno. "Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake." yaani, kutakasa ambako wanafanya viumbe wengineo ambao hawazungumzi lugha yako, lakini Yeye ajuaye zaidi ghaibu amevizunguka vyote. "Hakika Yeye ni Mstahamilivu na Mwenye kughufiria." Kwa maana hakumharakishia adhabu mwenye kusema kumhusu kauli ambayo mbingu na ardhi vinakaribia kupasuka kwa sababu yake na milima inakaribia kuangukia. Lakini yeye huwapa muhula na anawaneemesha, na anawapa salama, na anawaruzuku, na anawaita kwenye mlango wake ili watubie kutokana na dhambi hii kubwa, ili awape thawabu nyingi, na awasamehe dhambi zao. Na kama usingekuwa ustahamilivu wake na msamaha wake, mbingu zingeanguka juu ya ardhi, na asingeacha mnyama yeyote juu ya mgongo wake.