الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَّا تَجْعَلْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ فَتَقْعُدَ مَذْمُومًا مَّخْذُولًا ٢٢
{22} Yaani, usiitakidi kwamba kuna yeyote katika viumbe anayestahili chochote katika ibada, na wala usimshirikishe Mwenyezi Mungu na yeyote miongoni mwao. Kwa maana, hilo linasababisha kulaumiwa na kutupwa. Kwani Mwenyezi Mungu, Malaika wake, na Mitume wake walikataza ushirikina, na wakamlaumu mwenye kuufanya lawama kubwa zaidi, na wakaliwekea majina yanayolaumiwa na sifa mbaya ambazo yeyote mwenye kusifika nazo anakuwa ndiye mwenye kuelezeka kwa maelezo mabaya zaidi ya viumbe vyote na mwenye sifa mbaya zaidi kati yao, naye atatupwa katika mambo ya dini yake na dunia yake kulingana na kile alichoacha cha kujifungamanisha na Mola wake Mlezi. Na yeyote mwenye kufungamana na asiyekuwa Yeye, basi huyo ametupwa, na amekabidhiwa yule ambaye alijifungamanisha naye. Na hakuna hata mmoja wa viumbe anayeweza kumfaidi mtu yeyote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na kama vile mwenye kufanya mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ana lawama na kutupwa, basi mwenye kumpwekesha na akamfanyia Mwenyezi Mungu tu dini yake, na akafungamana naye na si mwingine, basi yeye atasifiwa, na kusaidiwa katika hali zake zote.