الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوٓا۟ إِلَّآ إِيَّاهُ وَبِٱلْوَٰلِدَيْنِ إِحْسَـٰنًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ ٱلْكِبَرَ أَحَدُهُمَآ أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَآ أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ٢٣
{23} Yeye Mtukufu alipokataza kumshirikisha na chochote, akaamrisha kupwekeshwa, akasema, " Na Mola wako Mlezi ameamrisha" yaani amri ya kisheria, "kuwa msimuabudu" yeyote katika wakazi wa ardhi na mbingu, walio hai na wafu, "isipokuwa Yeye tu" kwa sababu Yeye ni Mmoja, wa Pekee, Mkusudiwa, ambaye ana kila sifa ya ukamilifu, na katika sifa hiyo ana kubwa yake zaidi, kwa njia ambayo hakuna yeyote katika viumbe wake anayefanana naye. Naye ndiye anayeneemesha kwa neema za dhahiri na za ndani, mwenye kuzuia kila adhabu, Muumba, Mwenye kuruzuku, Mwendashaji wa mambo yote. Yeye ndiye ambaye ni wa pekee katika yote hayo, na wasiokuwa yeye hana chochote katika hayo. Kisha akataja baada ya haki yake, kutekeleza haki ya wazazi, akasema, "Na wazazi wawili muwatendee wema" yaani, watendeeni wema kwa nyanja zote za wema wa kimaneno na kimatendo. Kwa sababu wao ndio sababu ya kuwepo kwa mja, nao wanampenda na kumfanyia mwanao wema, na wako karibu sana naye, jambo ambalo linahitaji kuisisitiza haki zao na ulazima wa kuwafanyia wema. "Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili," yaani, wanapofikia umri huu ambao nguvu zao zinadhoofika na wanahitaji upole na ihsani kama inavyojulikana, "usiwaambie hata, 'Ah!'" Na hiki ndicho kiwango cha chini kabisa cha kuwaudhi, ambacho alikitumia kama mfano kwa mengineyo. Na maana yake ni kwamba usiwaudhi kwa hata udhia mdogo zaidi. "wala usiwakemee", na kuwaambia maneno makali. "Na uwaambie maneno ya heshima;" kwa maneno wanayoyapenda, na kuwa na adabu na upole kwa maneno laini, mazuri, yenye kuifurahisha mioyo yao, na kutuliza roho zao, na hayo yanatofautiana kulingana na hali tofauti tofauti, ada na nyakati mbalimbali.