يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًۢا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ إِن كُنَّا عَنْ عِبَادَتِكُمْ لَغَـٰفِلِينَ ٢٩
{29} "Basi Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi baina yetu na nyinyi. Hakika sisi tulikuwa hatuna habari na ibada yenu.” Hatukuwaamrisha kufanya hivyo, wala hatukuwaita kwa sababu yake, bali nyinyi mlimwabudu yule aliyewaita kwa ajili ya hilo. Naye ni Shetani, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Je, sikuwaagiza enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani? Kwani yeye hakika ni adui dhahiri kwenu.” Na akasema, “Na siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia Malaika: Je, hawa walikuwa wakiwaabudu nyinyi? Watasema: Umetakasika. Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao. Bali wao walikuwa wakiwaabudu majini, wengi wao wakiwaamini hao.” Kwa hivyo, Malaika watukufu, Manabii, mawalii (marafiki wa Mwenyezi Mungu), na mfano wao watajitenga na wale waliowaabudu Siku ya Qiyama, na watakataa madai ya kuwaita ili wawaabudu. Nao ni wakweli na wema katika hayo.