انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٨

وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ مَكَانَكُمْ أَنتُمْ وَشُرَكَآؤُكُمْ ۚ فَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ ۖ وَقَالَ شُرَكَآؤُهُم مَّا كُنتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ ٢٨

{28} Yeye Mtukufu anasema: "Na siku tutakapowakusanya wote;” yaani, tutakapowakusanya viumbe vyote kwa ajili ya miadi ya siku maalumu, na tutawahudhurisha washirikina na wale waliokuwa wakiabudu badala ya Mwenyezi Mungu. “Kisha tutawaambia wale walioshirikisha, "Simameni pahali penu nyinyi na washirika wenu." Yaani, bakieni pahali penu ili ipate kufanyika hukumu na kupambanua baina yenu na wao. “Kisha tutatenganisha baina yao,” yaani, tutawatenganisha kimwili na kimoyo, na kuwe na uadui mkubwa baina yao baada ya kwamba waliwapa katika dunia mapenzi ya dhati na juu zaidi, lakini mapenzi hayo na ulinzi yakageuka kuwa chuki na uadui. Na washirika wao wakajiweka mbali nao na wakasema, "Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi." Kwa maana, sisi tunamtakasa Mwenyezi Mungu kuwa na mshirika yeyote au mwenza.