انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٧

وَٱلَّذِينَ كَسَبُوا۟ ٱلسَّيِّـَٔاتِ جَزَآءُ سَيِّئَةٍۭ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ مَّا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِنْ عَاصِمٍ ۖ كَأَنَّمَآ أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ ٱلَّيْلِ مُظْلِمًا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ ٢٧

{27} Alipowataja wenza wa Pepo, akawataja wenza wa Moto, kwa hivyo akataja kwamba bidhaa zao ambazo walizichuma katika dunia hii ndiyo matendo mabaya yenye kumkasirisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa aina mbalimbali za ukafiri, na ukadhibishaji, na aina mbalimbali za maasia, kwa hivyo malipo yao ni mabaya mfano wake. Yaani, malipo yatakayowawiya mabaya kulingana na yale waliyoyafanya miongoni mwa mabaya kulingana na hali zao tofauti tofauti. "Na watafunikwa na madhila” katika mioyo yao na hofu ya adhabu ya Mwenyezi Mungu ambayo hakuna yeyote awezaye kuwaondolea wala hakuna mlinzi yeyote awezaye kuwalinda kutokana nayo. Na madhila hayo yatafika katika sura zao za nje, mpaka yawe meusi katika nyuso zao "kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio wenza wa Moto. Wao, humo watadumu;” basi ni tofauti gani iliyopo kati ya makundi mawili haya? Na ni umbali ulioje kati yao? "Zipo nyuso siku hiyo zitakazong'ara. Zikimwangalia Mola wao Mlezi. Na zipo nyuso siku hiyo zitakazokunjana. Zikijua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo." “Siku hiyo ziko nyuso zitakazonawiri. Zitacheka, zitafurahia. Na nyuso zingine siku hiyo zitakuwa na mavumbi. Giza totoro litazifunika. Hao ndio makafiri, waovu.”