يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ ٱلْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ ٢٦
{26} Na alipolingania kwenye nyumba ya amani, ni kana kwamba nafsi zilipata shauku juu matendo yenye kusababisha hilo na yenye kuwafikisha huko, kwa hivyo akajulisha juu yake kwa kauli yake: "Kwa wafanyao uzuri ni uzuri na zaidi.” Yaani, kwa wale waliofanya mazuri katika kumwabudu Muumba, kwa kumuabudu kwa namna ya kumchunga na kumsafishia ibada, na kufanya yale waliyoweza kufanya kwayo, na wakawafanyia uzuri waja wa Mwenyezi Mungu kwa yale wanayoweza miongoni mwa uzuri wa kikauli na wa kimatendo kama vile kutoa mali kwa uzuri na kufanya uzuri wa kimwili, na kuamrisha mema na kukataza maovu, kuwafundisha wasiojua, na kuwanasihi wapeanano migongo, na mambo mengineyo miongoni mwa njia mbalimbali za wema na ihsani. Basi hawa waliofanya uzuri wana uzuri zaidi, ambayo ni Pepo kamili katika uzuri wake, na ziada, ambayo ni kuutazama uso wa Mwenyezi Mungu, Mtukufu, na kusikia maneno Yake, na kupata ridha yake, na kufurahia kuwa karibu naye. Na kwa hivyo wakapata kitu cha juu zaidi ambacho wanakitamani wenye kutamani, na wanakiomba wenye kuomba. Kisha akataja kuondokewa kwao na kile wanachokihofu, akasema: "Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila.” Yaani, hawatapatwa na machukizo kwa namna yoyote ile. Kwa sababu machukizo yanapompata mwanadamu, yanaonekana kwenye uso wake na anabadilika na anahuzunika. Na ama hawa, basi ni kama Mwenyezi Mungu alivyosema kuwahusu, “Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema.” Hao ndio wenza wa Pepo watakaokaa humo milele. Hawataenda popote pengine, wala hawataondoka, wala hawatabadilika.