انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٥

وَٱللَّهُ يَدْعُوٓا۟ إِلَىٰ دَارِ ٱلسَّلَـٰمِ وَيَهْدِى مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ ٢٥

Na Mwenyezi Mungu alipotaja hali ya dunia hii, na matokeo ya starehe zake, akatamanisha juu ya nyumba yenye kubakia, akasema:

{25} Yeye Mtukufu aliwajumuisha waja wake katika kuwalingania kwenye nyumba ya amani, katika kuwahimiza juu yake na kuwatia moyo kufanya hivyo, na akafanya kuongoka kuwa maalumu kwa yule aliyetaka kumwokoa na kumchagua. Basi hii ni fadhila yake na wema wake, na Mwenyezi Mungu humchagua kumpa rehema zake amtakaye. Na huo ndio uadilifu wake na hekima yake, na hakuna mwenye hoja yoyote dhidi yake baada ya kubainisha na kuwatuma Mitume. Na Mwenyezi Mungu aliita Pepo kuwa ni nyumba ya amani kwa sababu ya usalama wake kutokana na balaa zote na mapungufu. Na hilo ni kwa sababu ya ukamilifu wa starehe zake, na ukamilifu wake, na kubakia kwake, na uzuri wake kwa kila njia.