انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣٠

هُنَالِكَ تَبْلُوا۟ كُلُّ نَفْسٍ مَّآ أَسْلَفَتْ ۚ وَرُدُّوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ مَوْلَىٰهُمُ ٱلْحَقِّ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ ٣٠

{30} Basi hapo, washirikina watajuta majuto yasiyoweza kuelezeka, na watajua kiwango cha yale waliyotanguliza katika matendo, na yale waliyofanya hapo zamani miongoni mwa sifa mbaya, na itawabainikia siku hiyo kwamba walikuwa waongo, na kwamba walikuwa wakimsingizia Mwenyezi Mungu. Ibaada zao zitapotea, na waabudiwa wao watatoweka, na zitakakika sababu zao na njia zao, na ndiyo maana Akasema, “Huko;” yaani, katika Siku hiyo “kila nafsi itayajua iliyoyatanguliza.” Yaani, zitayachunguza matendo yake na yale ziliyoyachuma, na zitafuatwa na malipo, na zitalipwa kulingana nayo, ikiwa ni ya heri, basi ni heri. Na ikiwa ni maovu, basi ni kwa uovu. “Na yote ya uongo waliyokuwa wakiyazua yatawapotea.” Yale waliyokuwa wakisema kwamba wanayofanya ya ushirikina ndiyo ya sahihi , na kwamba wale wanaoabudu badala ya Mwenyezi Mungu watawanufaisha na kuwaondolea adhabu.