انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢١

وَإِذَآ أَذَقْنَا ٱلنَّاسَ رَحْمَةً مِّنۢ بَعْدِ ضَرَّآءَ مَسَّتْهُمْ إِذَا لَهُم مَّكْرٌ فِىٓ ءَايَاتِنَا ۚ قُلِ ٱللَّهُ أَسْرَعُ مَكْرًا ۚ إِنَّ رُسُلَنَا يَكْتُبُونَ مَا تَمْكُرُونَ ٢١

{21} Yeye Mtukufu Anasema: "Na tunapowaonjesha watu rehema baada ya shida iliyowagusa” kama vile afya baada ya maradhi, na utajiri baada ya umasikini, na amani baada ya hofu, wanasahau yale yaliyowasibu miongoni mwa madhara, na hawamshukuru Mwenyezi Mungu juu ya maisha hayo ya raha na rehema. Bali wanaendelea na upotofu wao na njama zao, na kwa sababu ya hili ndiyo akasema: "Tazama, wanafanya njama katika Ishara zetu.” Yaani, wanafanya bidii katika batili ili waibatilishe haki kwayo. "Sema, “Mwenyezi Mungu ni Mwepesi zaidi wa kupanga njama” kwa maana njama haiwafikii isipokuwa wenyewe. Basi makusudio yao yanawarudia wao wenyewe, wala hawakuepuka lawama, bali Malaika wanawaandikia yake wanayoyafanya, na Mwenyezi Mungu atawahesabu kwayo, kisha Mwenyezi Mungu atawalipa kwayo malipo kamili zaidi.