يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
هُوَ ٱلَّذِى يُسَيِّرُكُمْ فِى ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ ۖ حَتَّىٰٓ إِذَا كُنتُمْ فِى ٱلْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِم بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا۟ بِهَا جَآءَتْهَا رِيحٌ عَاصِفٌ وَجَآءَهُمُ ٱلْمَوْجُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوٓا۟ أَنَّهُمْ أُحِيطَ بِهِمْ ۙ دَعَوُا۟ ٱللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ لَئِنْ أَنجَيْتَنَا مِنْ هَـٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ ٢٢ فَلَمَّآ أَنجَىٰهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِى ٱلْأَرْضِ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ ۗ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُم ۖ مَّتَـٰعَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ٢٣
{22-23} Yeye Mtukufu alipotaja kanuni ya jumla kuhusu hali za watu wakati wanapopatwa na rehema baada ya shida, na urahisi baada ya ugumu, akataja hali inayounga mkono hilo. Nayo ni hali yao katika bahari wakati wa michafuko yake kuhofu matokeo yake. Akasema: "Yeye ndiye anayewaendesha katika nchi kavu na baharini” kwa yale aliyowarahisishia miongoni mwa njia zinazoekwa kwa ajili yenu na akawaongoa kuzifikia. "Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri” zikiafikiana na wapendavyo, bila ya masumbuko wala ugumu, "na wakaufurahia" na wakawa na utulivu nao. Na huku wakiwa hivyo, ghafla ukawajia “upepo mkali” katika kuvuma kwake “na yakawajia mawimbi kutoka kila mahali, na wakaona kwamba wameshazungukwa.” Yaani, wakajua kuwa ni maangamivu, na wakati huo kukakatika kufungamana kwao na viumbe, na wakajua kuwa hakuna yeyote wa kuwaokoa na shida hii isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake. Wakamuomba "kwa kumpwekeshea yeye tu dini” na wakajiwekea ahadi kwa ufaradhinamna ya ulazima, na wakasema: “Ukituokoa na haya, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru. Na alipowaokoa, tazama, walikuwa wakifanya jeuri tena katika ardhi bila ya haki.” Yaani, walisahau shida hiyo, dua hiyo, na yale waliyojiwekea kwa namna ya ulazima juu ya nafsi zao, kwa hivyo wakamshirikisha Mwenyezi Mungu wale waliokiri kuwa hawawezi kuwaepusha kutokana na shida wala kuwakinga kutokana na matatizo. Basi kwa nini hawakumpwekeshea Mwenyezi Mungu ibada katika wakati wa raha kama vile walivyompwekesha katika nyakati za shida? Lakini jeuri hii yanarejea madhara yake juu yao, na ndiyo maana akasema: "Enyi watu! Hakika jeuri zenu zitawadhuru nyinyi wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu.” Yaani, matarajio yenu ya mwisho kwa jeuri yenu hiyo na kuwa kwenu mbali na kumpwekesha Mwenyezi Mungu ni kwamba mpate kitu katika mabaki ya dunia na heshima yake chache, ambayo yataisha haraka, na yote yatapita, kisha mtaondoka myaache hata msipotaka. "Kisha marejeo yenu ni kwetu” katika Siku ya Qiyama, "na hapo tutawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.” Na katika hili kuna onyo kubwa kabisa kwao juu ya kuendelea na matendo yao hayo.