يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَقُولُونَ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ ءَايَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ ۖ فَقُلْ إِنَّمَا ٱلْغَيْبُ لِلَّهِ فَٱنتَظِرُوٓا۟ إِنِّى مَعَكُم مِّنَ ٱلْمُنتَظِرِينَ ٢٠
{20} "Na wanasema;" yaani, hao wanaokadhibisha, wakaidi. "Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?” Wakimaanisha ishara wanazopendekeza wao ambazo wanazitaka wao. Kama vile kauli yao: "Mbona hakuteremshiwa Malaika akawa mwonyaji pamoja naye...?” Hadi mwisho wa aya hizi. Na kama kauli yake, “Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchemi katika ardhi hii...” hadi mwisho wa aya hizi. "Basi sema" uwaambie Wakikuomba Ishara: "Hakika mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu.” Yaani, Yeye ndiye amezizunguka kwa elimu hali za waja Wake, kwa hivyo anawaendesha kulingana na inavyohitaji elimu Yake kuhusiana nao, na hekima Yake ya ajabu. Na hakuna yeyote mwenye uendeshaji katika hukumu, wala ushahidi, wala lengo, wala sababu. "Basi nyinyi ngojeni, na mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.” Yaani, kila mmoja anamgonjelea mwenzake yale anayostahili. Basi ngojeni muone ni nani atakuwa na mwisho mwema.