Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ 4
(4) Kisha akasema “Na ambao wanayaamini yaliyoteremshwa kwako” nayo ni Qur-ani na Sunnah. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, “Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hekima.” Kwa hivyo, wachamungu huyaamini yote waliyokuja nayo Mitume, na wala hawatofautishi kati ya baadhi ya yale yaliyoteremshwa juu yake. Wakawa wanaamini baadhi yake na hawaamini baadhi yake, ima kwa kuyakanusha au kwa kuyafasiri kinyume na alivyokusudia Mwenyezi Mungu na Mtume wake; kama anavyofanywa hivyo mwenye kufanya miongoni mwa wazushi wanaoyafasiri maandiko yanayoashiria kinyume na kauli yao kwa ufasiri ambao, matokeo yake ni kutosadiki maana yake hata kama wanasadiki matamshi yake, basi hawakuamini kwayo imani ya kweli. Na kauli yake “na yaliyoteremshwa kabla yako” inakusanya kuamini katika vitabu vyote vilivyotangulia. Na kuamini katika vitabu kunajumuisha kuwaamini Mitume na yale yaliyomo (katika Vitabu hivyo) hasa Taurati, Injili na Zaburi. Na hii ni sifa maalumu ya Waumini, kuwa wanaamini katika vitabu vyote vilivyoteremshwa kutoka mbinguni, na katika Mitume wote, na hawatofautishi baina ya yeyote miongoni mwao. Kisha akasema “na Akhera wana yakini nayo.” Nayo “Akhera” ni jina la yatakayotokea baada ya kufa, na aliitaja hususan baada ya ujumla, kwa sababu kuamini katika Siku ya Mwisho ni moja katika nguzo za imani na kwa sababu ndicho chanzo kikuu zaidi cha kumfanya mtu kuwa na tamaa, hofu, na kutenda vitendo (vyema). Na "yakini" ni kuwa na elimu kamili ambayo haina shaka hata kidogo ndani yake, na ambayo inamlazimu mtu kutenda (matendo mema).