At-Tawba
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
كَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ كَانُوٓا۟ أَشَدَّ مِنكُمْ قُوَّةً وَأَكْثَرَ أَمْوَٰلًا وَأَوْلَـٰدًا فَٱسْتَمْتَعُوا۟ بِخَلَـٰقِهِمْ فَٱسْتَمْتَعْتُم بِخَلَـٰقِكُمْ كَمَا ٱسْتَمْتَعَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُم بِخَلَـٰقِهِمْ وَخُضْتُمْ كَٱلَّذِى خَاضُوٓا۟ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَـٰلُهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ 69 أَلَمْ يَأْتِهِمْ نَبَأُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَقَوْمِ إِبْرَٰهِيمَ وَأَصْحَـٰبِ مَدْيَنَ وَٱلْمُؤْتَفِكَـٰتِ ۚ أَتَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ ۖ فَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ 70
{69 - 70} Yeye Mtukufu anasema akiwatahadharisha wanafiki yasije yakawapata yale yaliyowapata umma waliokadhibisha kabla yao, “Kaumu ya Nuhu, na A'di, na Thamudi, na kaumu ya Ibrahim, na watu wa Madyana, na miji iliyopinduliwa chini juu?” Yaani, vijiji vya kaumu ya Lut. Kwani, wote “walijiwa na Mitume wao kwa hoja zilizo wazi.” Yaani, kwa haki iliyo wazi, ya peupe, yenye kubainisha hakika za mambo, lakini wakazikadhibisha, na yale aliyotuhadithia Mwenyezi Mungu yakawafikia. Basi nyinyi matendo yenu yanafanana na matendo yao. "Mmestareheka kwa fungu lenu;" yaani, fungu lenu katika dunia hii, basi mkalichukua kwa raha na matamanio, mkayapa mgongo yale yaliyokusudiwa kwalo, na mkajisaidia kwalo kumuasi Mwenyezi Mungu, wala azimio lenu na utashi wenu haukuzidi neema mlizopewa kama walivyofanya wale waliotangulia kabla yenu. “Na nyinyi mkazama katika maovu kama wao walivyozama;” yaani, mlizama katika batili na uongo na mkabishana kwa batili ili muiangushe kwayo haki. Haya basi ndiyo matendo yao na elimu zao: kufurahia kwa fungu lao na kuzama katika batili. Kwa hivyo walistahiki adhabu na maangamizo kama walivyostahiki wale waliokuwa kabla yenu miongoni mwa wale waliofanya kama kitendo chenu. Na ama Waumini, hata wakistareheka kwa fungu lao na kile walichopewa katika dunia hii, basi hayo ni kwa namna ya kutafuta msaada kwayo juu ya kumtii Mwenyezi Mungu. Na elimu zao, hizo ni elimu za Mitume. Nazo ni kufikia yakini katika matashi yote ya juu zaidi, na kujadiliana kwa haki ili kuivunja batili. Kauli yake, “Basi Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu” alipowafikishia adhabu yake namna alivyowafikishia. “lakini wao walikuwa wakijidhulumu wenyewe,” wa kuwa waliyafanyia ujasiri maasia yake, na wakawaasi Mitume wao, na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi.