Al-Muzzammil
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَىِ ٱلَّيْلِ وَنِصْفَهُۥ وَثُلُثَهُۥ وَطَآئِفَةٌ مِّنَ ٱلَّذِينَ مَعَكَ ۚ وَٱللَّهُ يُقَدِّرُ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ ۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۖ فَٱقْرَءُوا۟ مَا تَيَسَّرَ مِنَ ٱلْقُرْءَانِ ۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرْضَىٰ ۙ وَءَاخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِى ٱلْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ ٱللَّهِ ۙ وَءَاخَرُونَ يُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۖ فَٱقْرَءُوا۟ مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ ۚ وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَقْرِضُوا۟ ٱللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا۟ لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ وَٱسْتَغْفِرُوا۟ ٱللَّهَ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌۢ 20
{20} Mwenyezi Mungu alitaja mwanzoni mwa Sura hii kwamba alimuamuru Mtume wake kuswali usiku wa manane, thuluthi mbili yake, au thuluthi moja yake, na kanuni ya msingi ni kwamba umma wake wanapaswa kumfuata katika hukumu zote. Na alitaja mahali hapa kwamba yeye na kundi la waumini walitekeleza hilo. Na kwa kuwa kuainisha muda unaotakiwa hapa ni taabu kwa watu, alijulisha kwamba aliwafanyia rahisi sana katika hilo; akasema: "Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana." Yaani, anajua kiasi chake na kinachopita na kinachobakia katika viwili hivyo. "Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu" bila kuongezeka au kupungua. Kwa sababu hilo linahitaji kuwa macho na kufanya jitihada za ziada. Kwa hivyo, akakufanyieni wepesi na akakuamrisheni kufanya yale yaliyo mepesi kwenu, sawa iwe ni zaidi ya yale yaliyoamrishwa au kidogo kuliko yaliyoamrishwa, "basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur-ani" katika yale mnavyojua na ambavyo si vigumu kwenu. Na ndiyo maana akaamrishwa mwenye kuswali usiku kuswali maadamu bado ana ukakamavu. Lakini anapochoka au akaona uvivu au usingizi, basi na apumzike ili aijie swala kwa utulivu huku amepumzika. Kisha akataja baadhi ya sababu zinazofaa kupunguza huko, akasema: "Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa" ambao itakuwa vigumu kwao kuswali nusu ya usiku, au thuluthi mbili yake au thuluthi moja yake. Basi mgonjwa na aswali lililo jepesi kwake, na pia haamrishwi kuswali hali ya kuwa amesimama pale jambo hili linakuwa gumu kwake. Bali hata ikiwa ni vigumu kwake kuswali swala ya hiyari, basi ana haki ya kuiacha, na atapata thawabu kama alivyokuwa akifanya huku akiwa sahihi. "Na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu." Yaani, alijua kwamba wako wasafiri miongoni mwenu wanaosafiri kwa ajili ya biashara, ili wajitosheleze mbali na viumbe, na kujizuia mbali nao. Kwa hivyo, hali ya msafiri inafailia afanyiwe wepesi, na ndiyo maana amefanyiwa wepesi katika swala ya faradhi kwa ruhusiwa kuunganisha swala mbili kwa wakati mmoja na kufupisha swala za rakaa nne. Vile vile "wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo." Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja wepesishaji mara mbili. Wepesishaji kwa ajili ya mtu aliye sahihi asiyekuwa safarini. Huyo anapaswa kuzingatia ukakamavu wake bila ya kumtwisha mzigo wa kuswali muda mrefu. Bali atajitahidi kuswali swala bora zaidi, ambayo ni thuluthi ya usiku baada ya nusu ya kwanza ya usiku. Na wepesishaji kwa ajili ya mgonjwa na msafiri, iwe safari yake iwe ni kwa ajili ya biashara au kwa ajili ya ibada, kama vile jihadi, Hija, au kitu kingine. Yeye [pia] na azingatie kile ambacho hakimpi mzigo mzito. Basi sifa njema ni za Mwenyezi Mungu na kutajwa kwa uzuri. Kwani hakutuwekea ugumu wowote katika dini, bali aliifanya sheria yake kuwa nyepesi, na akazingatia hali za waja wake na masilahi ya dini yao, miili yao na dunia yao. Kisha akawaamrisha waja kufanya ibada mbili, nazo ndizo mama za ibada zote na nguzo zake: kusimamisha swala ambayo bila ya hiyo dini hainyooki, na kutoa zaka ambayo ni ushahidi wa imani na kwayo faraja inapatikana kwa masikini na mafukara. Akasema: "na mshike Sala" kwa nguzo zake, na mipaka yake, na masharti yake, na vyote vinavyoikamilisha. "Na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema." Yaani, ambao umekusudiwa kwa huo uso wa Mwenyezi Mungu peke yake, kwa nia ya ukweli, na kuzipa nguvu roho, na mali nzuri, na hili linajumuisha sadaka ya faradhi na ile inayopendekezwa. Kisha akahimiza kufanya heri kwa ujumla na vitendo vyake, akasema: "Na kheri yoyote mnayoitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana," jema moja kwa mara kumi mfano wake hadi mizidisho mia saba, hadi mizidisho mara nyingi. Na ajue kwamba uzito wa chembe wa wema katika makazi haya unalingana mizidisho mara nyingi ya dunia hii na vilivyomo katika nyumba ya neema ya milele miongoni mwa starehe na matamanio, na kwamba heri na wema katika dunia hii ndiyo kiini cha heri na wema katika nyumba ya daima, mbegu yake, asili yake na msingi wake. Basi ninasikitika sana juu ya nyakati zilizopita katika hali ya kughafilika! Na lo, ni majuto yaliyoje kwa nyakati zilizotumiwa katika mambo mengine yasiyo ya matendo mema! Na lo, ni majuto yaliyoje kwa mioyo ambayo mawaidha ya Muumba wao hayakuwa na athari yoyote ndani yake, na ambayo hamu ya Yule aliye na huruma zaidi kwao hata kuliko nafsi zao wenyewe haikuwaingia! Basi ewe Mwenyezi Mungu ni zako sifa njema, na ni kwako ndiko pa kulalamikia, na wewe ndiye unayeombwa msaada, na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwako. "Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu." Kuna faida kubwa katika kuamrisha kuomba msamaha baada ya kuhimiza vitendo vya utiifu na wema, na hilo ni kuwa mja hakosi kuwa na mapungufu katika yale aliyoamrishwa kuyafanya: Ima kwa kutoyafanya kabisa, au kayafanya kwa njia pungufu. Kwa hivyo akaamrishwa kurekebisha hayo kwa kuomba msamaha. Kwani mja anatenda madhambi nyakati za mchana na usiku. Na Mwenyezi Mungu asipomfunika kwa rehema na msamaha wake, basi atakuwa ameangamia.
Imekamilika tafsiri yake, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.