İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Qalam
Sure 68

Al-Qalam

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

48–50. âyetler

فَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ مَكْظُومٌ 48 لَّوْلَآ أَن تَدَٰرَكَهُۥ نِعْمَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ لَنُبِذَ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ مَذْمُومٌ 49 فَٱجْتَبَـٰهُ رَبُّهُۥ فَجَعَلَهُۥ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ 50

{48 - 50} Basi hakikubakia isipokuwa kuwa na subira juu ya maudhi yao, na kustahimili yale yatokayo kwao, na kuendelea katika kuwalingania, ndiyo maana akasema: "Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi" Yaani, kile alichohukumu kisheria na kulingana na mipango yake. Kwani hukumu inayohusiana na mipango ya Mwenyezi Mungu ni lazima mtu awe mvumilivu juu ya chenye kumdhuru katika hukumu hiyo, wala haikabiliwi kwa ghadhabu na hofu na kutokuwa na subira. Nayo hukumu ya kisharia inakabiliwa kwa kuikubali, kusalimu amri, na kufuata [kikamilifu]. Na kauli yake: "wala usiwe kama mmezwa na samaki." Naye alikuwa nabii Yunus bin Matta, rehema na amani ziwe juu yake. Yaani, usijifananishe naye katika hali iliyompelekea kunaswa ndani ya tumbo la nyangumi, nayo ni kutokuwa na subira kwa watu wake, subira inayotakiwa kwake, na kwenda kwake kwa hasira akimwacha Mola wake Mlezi. Akapanda baharini, na watu wa merikebu ilipolemewa na watu wake, wakapiga kura ili ijulikane ni nani wao watamtupa ndani ya bahari. Ili merikebu ipate kuwa nyepesi, basi kura ikamwangukia, na nyangumi akammeza huku ni wa kulaumiwa. Na kauli yake: "aliponadi naye kazongwa." Yaani, alipokuwa tumboni mwake, alikuwa akihuzunika juu yake, au aliita hali ya kuwa amehuzunika na kuzongwa, na akasema: 'Hapana mungu ila Wewe, umetakasika. Hakika mimi nimekuwa katika madhalimu.' Basi Mwenyezi Mungu akamwitikia, na nyangumi huyo akamtema nje ya tumbo lake ufukweni patupu, hali yu mgonjwa. Na Mola wake Mlezi akamuotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye. Ndiyo maana akasema hapa, "Kama isingelimfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angelitupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa," lakini Mwenyezi Mungu akamfunika kwa rehema yake, na akatemwa hapo huku anasifiwa kwa uzuri, na hali yake ikawa bora kuliko hali yake ya awali, ndiyo maana akasema: "Lakini Mola wake Mlezi alimteua" na akamtakasa kutokana na kila uchafu, "na akamfanya miongoni mwa watu wema" katika matendo yao, maneno yao, nia zao na hali zao.