İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Jumu'a
Sure 62

Al-Jumu'a

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 5

مَثَلُ ٱلَّذِينَ حُمِّلُوا۟ ٱلتَّوْرَىٰةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ ٱلْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًۢا ۚ بِئْسَ مَثَلُ ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ ۚ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ 5

{5} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja neema yake juu ya umma huu ambao alituma miongoni mwao Nabii asiyejua kusoma na kuandika, na yale aliyowapa Mwenyezi Mungu wao tu ya sifa maalumu, ambayo hakuna anayeweza kuwafikia katika hayo, nao ni umma wasiojua kusoma na kuandika, waliopiku wa kale na wa mwisho, hata Watu wa Kitabu wanaojidai kuwa ni wanavyuoni wacha Mungu na makohani walio mbele sana, akataja wale ambao Mwenyezi Mungu aliwabebesha Taurat miongoni mwa Mayahudi na Wakristo, na akawaamrisha waijifunze na kuifanyia kazi, lakini hawakuibeba na hawakufanya yale waliyobebeshwa, kwamba hawana ubora, na kwamba mfano wao ni kama punda anayebeba juu ya mgongo wake vitabu vya elimu; Je, punda huyo anafaidika na vitabu hivyo vilivyo juu ya mgongo wake? Je, ubora wowote utampata kwa sababu hilo? Au fungu lake katika hilo ni kuvibeba tu? Huu ndio mfano wa wanavyuoni wa Watu wa Kitabu ambao hawakutenda kulingana na yale yaliyomo ndani ya Taurati ambayo kubwa yake zaidi na tukufu yake zaidi ni ile amri ya kumfuata Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kupeana bishara ya kuja kwake na kuamini aliyoyaleta katika Qur-ani. Basi je, kuna yeyote ambaye hizi ndizo sifa zake kutoka katika Taurati isipokuwa kuambulia patupu, hasara, kusimamishiwa hoja dhidi yake? Mfano huu unaingiliana vyema na hali zao. "Mfano muovu mno wa watu waliokadhibisha" Aya zetu zinazoashiria ukweli wa Mtume wetu na usahihi wa yale aliyokuja nayo, "na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu" kufikia masilahi yao maadamu dhuluma na ukaidi bado ndizo sifa zao.