As-Saff
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كُونُوٓا۟ أَنصَارَ ٱللَّهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّـۧنَ مَنْ أَنصَارِىٓ إِلَى ٱللَّهِ ۖ قَالَ ٱلْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ ٱللَّهِ ۖ فَـَٔامَنَت طَّآئِفَةٌ مِّنۢ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ وَكَفَرَت طَّآئِفَةٌ ۖ فَأَيَّدْنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا۟ ظَـٰهِرِينَ 14
{14} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Enyi mlioamini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu." Yaani, kwa kauli na vitendo, kwa kushikamana na dini ya Mwenyezi Mungu, na kufanya bidii ya kuitekeleza kwa wengine, na kufanya jihadi kwa miili na mali dhidi ya mwenye kuikaidi na kuikataa. Na mwenye kuunga mkono batili kwa elimu anayodai kwamba anayo, na anaikanusha haki kwa kuiangusha hoja yake, na kusimamisha ushahidi dhidi yake, na kuonya dhidi yake, na mwenye kuunga mkono Dini ya Mwenyezi Mungu kwa kujifunza Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake na kuyahimiza hayo na kuamrisha mema na kukataza maovu. Kisha Mwenyezi Mungu akawachochea Waumini wawaige watu wema waliokuwa kabla yao kwa kusema: "Kama alivyosema Isa bin Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: 'Ni nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu?'" Yaani, aliwaambia kwa njia ya kuwatanabahisha: Ni nani atakayenisaidia na kusimama pamoja nami katika kuiunga mkono dini ya Mwenyezi Mungu na aingie kwenye maingilio yangu na kutoka kupitia pale ninapotokea? Kisha wanafunzi wake wakaharakisha kusema: "Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu!" Basi [Isa], amani iwe juu yake, akaendelea na [maamrisho ya Mwenyezi Mungu na] kuunga mkono dini ya Mwenyezi Mungu, yeye na wale wanafunzi waliokuwa pamoja naye. "Basi kundi moja la Wana wa Israili liliamini" kwa sababu ya mwito wa Isa na wanafunzi wake, "na kundi jingine lilikufuru." Hawakukubali wito wao. Kwa hivyo, Waumini wakapigana dhidi ya makafiri. "Basi tukawaunga mkono wale walioamini dhidi ya maadui zao" kwa kuwatia nguvu na tukawanusuru dhidi yao, "wakawa wenye kushinda" dhidi yao. Basi enyi umma wa Muhammad! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu na watetezi wa dini yake. Mwenyezi Mungu atakusaidieni kama alivyowasaidia wale waliokuwa kabla yenu, na atakupeni ushindi juu ya adui yenu.
Imekamilika tafsiri ya sura hii, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.