İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Hadid
Sure 57

Al-Hadid

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 10

وَمَا لَكُمْ أَلَّا تُنفِقُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلِلَّهِ مِيرَٰثُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ لَا يَسْتَوِى مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ ٱلْفَتْحِ وَقَـٰتَلَ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ ٱلَّذِينَ أَنفَقُوا۟ مِنۢ بَعْدُ وَقَـٰتَلُوا۟ ۚ وَكُلًّا وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلْحُسْنَىٰ ۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ 10

{10} "Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu?" Yaani, ni nini kinachokuzuieni kutumia mali zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu? Nao ni njia za wema zote, na kinawafanya kuwa mabahili. "Na" hali ni kwamba hamna chochote, bali "urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu." Kwani mali zote zitatoka katika mikono yenu au nyinyi wenyewe mtaziacha, kisha umiliki wake utamrudia mmiliki wake hasa, Mwenye baraka nyingi, Mtukufu. Kwa hivyo, tumieni fursa kutoa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu madamu bado mna mali mikononi mwenu Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja maelezo ya kina ya matendo kulingana na hali na hekima ya kimwenyezi Mungu, akasema: "Hawawi sawa miongoni waliotoa kabla ya Ushindi na wakapigana vita. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao walitoa baadaye na wakapigana." Kinachokusudiwa hapa na ushindi ni ule ushindi wa Al-Hudaybiyya, yalipofanyika mapatano ya amani baina ya Mtume na Makureshi, ambao ulikuwa katika ushindi mkubwa zaidi kuliko ambao ndani yake ulienea Uislamu, kuchanganyika Waislamu na makafiri, na kuilingania dini bila upinzani. Basi tangia wakati huo watu wakaingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi, na Uislamu ukapata nguvu kubwa sana, na kabla ya ushindi huu, Waislamu hawakuwa na uwezo wa kuilingania dini katika sehemu nyinginezo isipokuwa katika maeneo ambayo watu wake walikuwa wamesilimu kama vile Madina na viunga vyake. Na watu waliosilimu wa Makka na maeneo mengineyo ya washirikina walikuwa wakiadhibiwa na kuogopa. Kwa hivyo akawa aliyesilimu kabla ya ushindi [na akatoa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu] na akapigana vita ni mwenye daraja kubwa zaidi na malipo kuliko yule ambaye hakuwa amesilimu, kupigana vita na kutoa mali isipokuwa baada ya hayo, kama inavyotakiwa na hekima, na ndiyo kwa sababu wengi wa waliotangulia na masahaba bora zaidi walisilimu kabla ya ushindi huu. Na kwa kuwa kuboresha kati ya mambo kunaweza kusababisha ifahamike kwamba kuna upungufu na dosari katika kile ambacho hakikuboreshwa, Mwenyezi Mungu akaondoa hili kwa kauli yake: "Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema." Yaani, wale waliosilimu, wakapigana, na wakatoa mali zao kabla ushindi, na baada yake, wote Mwenyezi Mungu aliwaahidi bustani za mbinguni. Hii inaashiria fadhila za Maswahaba wote, Mungu awe radhi nao, kwani Mwenyezi Mungu alishuhudia imani yao na kuwaahidi Pepo. "Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda." Atamlipa kila mmoja wenu kwa anayoyajua katika matendo yake.