Al-Qamar
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
ٱقْتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلْقَمَرُ 1
{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kwamba Saa - ambayo ni Kiyama - imekaribia, na wakati wa kuja kwake umefika, lakini pamoja na haya, wale wanaokadhibisha wanaendelea tu kuikadhibisha na wala hawajiandai kwa ajili ya kuteremka kwake. Na Mwenyezi Mungu anawaonyesha miongoni mwa ishara kubwa zinazoonyesha kutokea kwake, ambazo mfano wake wameshaamini watu wengine. Basi katika ishara kubwa zaidi zinazoashiria usahihi wa yale aliyokuja nayo Muhammad bin Abdullah – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie ni pale wakadhibishaji walipomtaka awaonyeshe muujiza wa kuunga mkono usahihi na ukweli wa kile alichokileta, yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie - akauashiria mwezi, nao ukagawanyika sehemu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kipande kimoja kilikuwa juu ya mlima unaoitwa Abu Qubays, na kipande kingine kikawa juu ya mlima unaoitwa Qu’ayqa'an, ilhali washirikina na wengineo wanaitazama ishara hii kubwa iliyotokea katika ulimwengu wa juu, ambayo mtu hawezi kuficha uhalisia wake na kuchukulia kwamba ni mazingaumbwe. Basi wakaona jambo ambalo hawakuwahi kuona mfano wake, bali hata hawakuwahi kusikia kwamba kuna hata mmoja wa Mitume kabla yake aliyefanya mfano wake. Basi wakalistaajabia hilo, lakini Imani haikuingia nyoyoni mwao, na Mwenyezi Mungu hakuwatakia heri, kwa hivyo wakaingiwa na hofu na kukimbilia jeuri yao na kupindukia kwao mipaka, na wakasema: ‘Muhammad ameturoga!’ Lakini alama ya hilo ni kuwa mtamuuliza aliyekujieni kutoka safarini. Kwani hata kama ataweza kuwaroga nyinyi, basi hataweza kumroga yule ambaye yuko hapa akiangalia kama nyinyi. Basi wakawauliza kila aliyewajia, nao wakawaambia kwamba kweli hilo lilitokea, lakini hawa wakasema: "Huu ni uchawi tu unazidi kuendelea!" Muhammad alituroga na akaroga watu wengine pia!! Hili ni katika uwongo ambao hauenei isipokuwa kwa watu wapumbavu zaidi na waliopotoka zaidi mbali na uwongofu na akili.