Al-Maaida
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
لَيْسَ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوٓا۟ إِذَا مَا ٱتَّقَوا۟ وَّءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ ثُمَّ ٱتَّقَوا۟ وَّءَامَنُوا۟ ثُمَّ ٱتَّقَوا۟ وَّأَحْسَنُوا۟ ۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلْمُحْسِنِينَ 93
{93} Wakati kuharamishwa kwa mvinyo kulipoteremka na katazo la mwisho na kutilia mkazo juu yake, baadhi ya Waumini walitamani kujua hali ya ndugu zao waliokufa katika Uislamu kabla ya kuharamishwa kwa mvinyo hali ya kuwa wanainywa. Basi Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba; "Hakuna ubaya juu ya wale walioamini na wakatenda mema; yaaani, kosa na dhambi "kwa vile walivyovila (zamani)" kutokana na mvinyo na kamari kabla ya kuharamishwa kwake. Na pindi kukataza kwa ubaya kulikuwa kunajumuisha hayo yaliyotajwa na mengineyo, akalifungia hilo kwa kauli yake; "maadamu wakimcha Mungu na wakiamini na wakitenda mema." Yaani, kwa sharti kwamba wataacha maasia na kumwamini Mwenyezi Mungu imani ya sahihi yenye kuwafanya kutenda mema, kisha wakaendelea kufanya hivyo. Vinginevyo, mja anaweza kusifika kwa hilo katika wakati mmoja na siyo mwingine, kwa hivyo haitoshi mpaka awe hivyo, mpaka ajiwe na mauti yake; na aendelee kudumu katika wema wake. Kwa maana Mwenyezi Mungu anawapenda wanaofanya wema katika kumwabudu Muumba, wanaofanya wema katika kuwanufaisha waja wake. Na inaingia katika Aya hii tukufu mwenye kula kilichoharamishwa, au akafanya kitu kinginecho baada ya kuharamishwa kwake, kisha akakiri dhambi yake, na akatubia kwa Mwenyezi Mungu, na akamcha Mwenyezi Mungu, na akaamini, na akatenda mema. Basi Mwenyezi Mungu atamfutia mabaya, na itamwondolea dhambi katika hilo.