İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
Sure 5

Al-Maaida

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 6

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا قُمْتُمْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ فَٱغْسِلُوا۟ وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى ٱلْمَرَافِقِ وَٱمْسَحُوا۟ بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى ٱلْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَٱطَّهَّرُوا۟ ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰٓ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَآءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ ٱلْغَآئِطِ أَوْ لَـٰمَسْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمْ تَجِدُوا۟ مَآءً فَتَيَمَّمُوا۟ صَعِيدًا طَيِّبًا فَٱمْسَحُوا۟ بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَـٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُۥ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ 6

{6} Hii ni Aya kubwa ambayo imejumuisha hukumu nyingi, na tutataja miongoni mwake aliyoyafanya Mwenyezi Mungu kuwa mepesi na sahali. Moja yake ni kwamba, mambo haya yaliyotajwa ndani yake kuna kwamba kuyafuata na kuyafanyia kazi ni miongoni mwa yale yanayoambatana na imani ambayo haitimii isipokuwa kwayo. Kwa sababu aliyaanzisha kwa kauli yake "Enyi mlioamini..." mpaka mwisho wake. Yaani, Enyi mlioamini, fanyeni kulingana na matakwa ya imani yenu kwa yale tuliyowawekea kama sheria. La pili ni amri ya kusimamisha swala kwa kauli yake, "Mnaposimama kwa ajili ya swala." La tatu ni amri ya kuweka nia kwa ajili ya swala, Kwa kauli yake, "Mnaposimama kwa ajili ya swala." Yaani, kwa kuikusudia na kuiwekea nia. La nne ni sharti la kufanya usafi ili swala iwe sahihi. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliamrisha hilo wakati wa kusimama kwa ajili ya swala. Na kanuni ya asili katika amri ni kwamba ni wajibu. La tano ni kwamba, kufanya usafi siyo wajibu kwa kuingia tu wakati wa swala. Bali ni wajibu wakati wa kutaka kuswali. La sita ni kwamba, kila kinachoitwa swala miongoni mwa zile za faradhi, na za sunna, na faradhi za kutosheleza, na swala ya jeneza ni sharti kufanya usafi kwa ajili yake. Hata kusujudu tu kwa mujibu wa wanachuoni wengi; kama vile kusujudu kwa sababu ya kusoma Qur-ani na kwa ajili ya kushukuru. Ya saba ni kwamba, amri ya kuosha uso. Ambayo ni sehemu inayotumika kumuelekea mtu kuanzia kwenye sehemu ya kawaida zinapoota nywele za kichwa hadi sehemu ya shavu na kidevu kiurefu, na kutoka kwenye sikio hadi kwenye sikio kiupana. Na inaingia ndani yake kusuuza mdomo na kupandisha maji kwenye pua kwa mujibu wa Sunnah. Na inaingia ndani yake nywele zilizo juu yake, lakini ikiwa ni nyepesi, basi ni lazima kuyafikisha maji kwenye ngozi. Na kama ni nyingi, basi itatosheleza kwa juu yake tu. La nane ni Amri ya kuosha mikono miwili, na kwamba kipimo chake ni hadi kwenye viwiko. Na "hadi" kama walivyosema wafasiri wengi inamaanisha 'pamoja na.' Kama kauli yake Yeye Mtukuf, "Wala msile mali zao pamoja na mali zenu." Na kwa sababu wajibu hautimii isipokuwa kwa kuosha viwiko vyote. La tisa ni amri ya kupangusa kichwa. La kumi ni kwamba, ni wajibu kukipangusa chote. Kwa sababu herufi 'ba' siyo yenye maana ya baadhi. Lakini ni yenye maana ya kuambatanisha, na kwamba inajumuisha kupangusa kichwa chote. La kumi na moja ni kwamba, inatosha kupangusa kwa namna yoyote kwa mikono yake miwili au mkono mmoja au kwa kitambaa, au kipande cha mti au mfano wake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuachilia kupangusa, na hakukufungia katika namna fulani, basi hilo likaonyesha kuachiliwa kwake. La kumi na mbili ni kwamba la wajibu ni kupangusa. basi ikiwa atakiosha kichwa chake na hakupangusa kwa mkono wake juu yake, basi halitoshi. Kwa sababu hakufanya kile Mwenyezi Mungu alimwamrisha. La kumi na tatu ni amri ya kuosha miguu mpaka vifundoni. Na inasemwa kuhusiana nayo miwili yale yanayosemwa kuhusu mikono miwili. La Kumi na Nne ni kwamba, ndani yake kuna jibu kwa Ar-Rafidha kuhusu kusoma kwa wengi wa wanachuoni kwa kuweka fatiha juu ya herufi laam (katika neno arjulakum, yani miguu yenu). Na kwamba hairuhusiki kuipangusa madamu iko wazi. La kumi na tano ni kwamba, ndani yake kuna ishara juu ya kupangusa juu ya soksi kwenye kisomo cha kuweka kasra juu ya laam katika "na miguu yenu." Na kinakuwa kila kisomo kati ya visomo hivi viwili kina maana yake. Basi kwa kisomo cha fatiha, kuna kuiosha ikiwa iko wazi, na kwa kisomo cha kasra, kuna kuipangusa ikiwa imefunikwa Khuff (soksi). La kumi na sita ni amri kufanya mpangilio katika kutawadha. Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alivitaja kwa mpangilio. Na kwa sababu aliingiza kinachopanguswa - nacho ni kichwa - kati ya viwili vinavyooshwa, na halijajulikana kuwa na faida yoyote isipokuwa mpangilio. La kumi na saba ni kwamba, mpangilio ni maalumu tu kwa vile viungo vinne vilivyotajwa katika aya hii. Na ama mpangilio kati ya kusukutua na kuingiza maji puani, na kati ya uso au mkono au mguu wa kulia na wa kushoto, hilo si wajibu. Bali inapendekezwa kusukutua na kupandisha maji puani kabla ya kuosha uso. Na kutanguliza cha kulia kabla ya cha kushoto katika mkono na mguu, na kutanguliza kupangusa kichwa mbele ya kupangusa masikio. La kumi na nane ni amri ya kufanya wudhuu upya wakati wa kila swala. Ili kupatikane picha ya kile kilichoamrishwa. La kumi na tisa ni Amri ya kuosha kutoka kwenye uchafu. La ishirini ni kwamba, ni lazima ni kuuosha mwili wote. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alifungamanisha kufanya usafi huu na mwili, na hakufanya kitu fulani kuwa mahususi kwa hilo kando na kingine. La ishirini na moja ni Amri ya kuosha nywele za nje na za ndani wakati wa janaba. La ishirini na mbili ni kwamba, hadathi ndogo inaingia katika hadathi kubwa, na inamtosha mwenye mawili hayo kuweka nia kisha aufikishie mwili wake wote maji. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hakutaja isipokuwa kufanya twahara tu, wala hakutaja kuwa atarudia kutawadha. La ishirini na tatu ni kwamba, sifa ya kuwa na janaba inampata aliyetoa manii hali ya kuwa yuko macho, au katika usingizi au alifanya jimai bila ya kutoa manii La ishirini na nne ni kwamba, mwenye kukumbuka kuwa alitokwa na manii lakini hakupata unyevunyevu, basi huyo halazimiki kuoga, janaba haikupatikana kwake kwa uhakika. La ishirini na tano ni kutajwa kwa neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake kwa kuwawekea sheria ya Tayammum. La ishirini na sita ni kwamba, katika sababu za kuruhusiwa kwa Tayammam ni kuwepo kwa maradhi ambayo yatamdhuru kwa kujiosha kwa maji, kwa hivyo inaruhusima kwake kufanya tayammam. La ishirini na saba ni kwamba, miongoni mwa sababu za kuruhusiwa kwake ni: Kusafiri na kwenda haja ndogo na kubwa kama hakuna maji. Kwa hivyo Maradhi yanafanya inaruhusika kutayammamu pamoja na kuwepo maji, kwa sababu yanakuwepo madhara kwa sababu yake. Na mengineyo yanafanya inaruhsika kwa sababu ya kutokuwepo kwa maji hata ikiwa ni katika hali ya kuwa nyumbani. La ishirini na nane ni kwamba, chenye kutoka katika njia mbili kama vile mkojo na kinyesi vinaharibu wudhuu. La ishirini na tisa ni kwamba, waliitumia kama ushahidi wale waliosema: Hayaharibu wudhuu isipokuwa mambo haya mawili tu. Kwa hivyo haiharibiki kwa kugusa sehemu za siri au kitu kingine chochote. La thelathini ni inapendekezwa kutumia tasfida kwa kitu ambacho kinachukuliwa kuwa ni kichafu kukitamka, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Au mmoja wenu akija kutoka kwenye choo." La thelathini na moja ni kwamba, kumgusa mwanamke kwa raha na matamanio kunabatilisha wudhuu. La thelathini na mbili ni kwamba, ni sharti kutokuwepo maji ili tayammam ikubalike. La thelathini na tatu ni kwamba, pamoja na uwepo wa maji, hata ikiwa ni ndani ya sala, tayammam inabatilika. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliiruhusu tu wakati wa kutokuwepo maji. La thelathini na nne ni kwamba, ikiwa wakati utaingia hali ya kuwa hana maji pamoja naye; basi inamlazimu kuyatafuta katika safari yake na katika kile kilicho karibu naye. Kwa sababu haiwezi kusemwa: Hakupata, kwa yule ambaye hakutafuta. La thelathini na tano ni kwamba, mwenye kupata maji ambayo hayatoshi baadhi ya kujisafisha kwake. basi, yeye inamlazimu kuyatumia kisha afanye tayammam baada ya hapo. La thelathini na sita ni kwamba, maji yaliyobadilika kwa sababu ya kuchanganyika na kitu safi yanatangulizwa mbele ya kutayammam. Yaani, ni safi; kwa sababu maji ya yaliyobadilika ni maji, kwa hivyo yanaingia katika kauli yake, "Na hamkupata maji." La Thelathini na saba ni kwamba, ni lazima kuweka nia ya kutayammam. Kwa sababu ya kauli yake, "Basi kusudieni." La thelathini na nane ni kwamba, inatosha kufanyia Tayammam kila kilichoinuka juu ya uso wa ardhi kama vile udongo na vinginevyo. Na inakuwa kwa maana hii kauli yake, "Basi pakeni nyuso zenu na mikono yenu katika hilo." Ima ni katika mlango wa aghalabu, na kwamba aghalabu huwa na vumbi inayopanguswa kwayo na inajipaka kwenye uso na mikononi miwili, na ima ni kuelekeza kwa lililo bora zaidi. Na kwamba ikiwezekana udongo wenye vumbi, basi hilo ndilo bora zaidi. La thelathini na tisa ni kwamba, si sahihi kufanya Tayammamu kwa udongo najisi. Kwa sababu huo si mzuri, bali ni mbaya. La arobaini ni kwamba, katika tayammam inapanguswa kwenye uso, na mikono miwili pekee, na siyo viungo vingine vyote. La arobaini na moja ni kwamba kauli yake, "kwenye nyuso zenu," inajumuisha uso wote, na kwamba aupanguse wote. Hata hivyo, imesamehewa kuingiza udongo katika mdomo, na pua, na chini ya nywele, hata ikiwa ni kidogo tu. La arobaini na mbili ni kwamba, mikono miwili inapanguswa hadi kwenye viwiko tu, kwa sababu mikono miwili inapotajwa bila ya kuzuiwa inakuwa na maana hiyo. Na lau ingehitajika kufikisha kupangusa kwenye dhiraa, basi Mwenyezi Mungu angeizuilia hivyo, kama alivyoifungia katika kutawadha. La arobaini na tatu ni kwamba Aya hii ni ya jumla katika kuruhusiwa tayammam kwa sababu ya hadathi zote; hadathi kubwa na hadathi ndogo. bali hata najasa ya mwili. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliifanya kuwa badala ya kufanya usafi kwa maji, na akaiacha aya bila ya kuifungia. Na Inaweza kusemwa: Hakika Najisi ya mwili haingii ndani ya hukumu ya tayammam. Kwa sababu muktadha huu ni katika hadathi mbalimbali, na hii ndiyo kauli ya wanachuoni walio wengi. La arobaini na nne ni kwamba, pahali pa tayammamu katika hadathi ndogo na kubwa ni sawa, napo ni uso na mikono. La arobaini na tano ni kwamba, iwapo mwenye hadathi mbili atakusudia kufanya tayammam kwa niaba ya mbili hizo, basi inatosheleza; kwa kuchukua kutoka katika maana ya jumla ya Aya na kutofungiwa kwake. La arobaini na sita ni kwamba, Inatosha kupangusa kwa chochote kile, kwa mkono wake au kinginecho. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisema, "Basi panguseni," na wala hakutaja cha kupangusia, basi hilo likaashiria kuruhusiwa kwake kwa kila kitu. La arobaini na saba ni sharti la kufanya utaratibu katika tayammum kama unavyotakiwa katika wudhuu, na kwa sababu Mwenyezi Mungu alianza na kupangusa kwenye uso kabla ya kuipangusa kwenye mikono. La arobaini na nane ni kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu katika yale aliyotuwekea miongoni mwa hukumu, hakutuwekea ndani yake ugumu, wala dhiki, wala mashaka, wala taabu. Bali ni rehema kutoka kwake kwa waja wake ili awatakase na kuwatimizia neema zake. Na haya ndiyo hilo. La arobaini na tisa ni kwamba, usafi wa nje kwa maji na udongo unakamilisha usafi wa ndani kwa tauhidi na toba ya kweli. La hamsini ni kwamba, usafi wa tayammam hata kama hauna unadhifu, na usafi unatambulika kwa hisia na kuona. Lakini ndani yake kuna usafi wa kimaana unaotokana na kufuata amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. La hamsini na moja ni kwamba, mja anapaswa kutafakari hekima na siri katika sheria za Mwenyezi Mungu kuhusu usafi na mambo mengine, ili azidi maarifa na elimu, na azidi shukurani kwa Mwenyezi Mungu na kumpenda juu ya hukumu alizoziweka kama sheria ambazo zinamfikisha mja kwenye vyeo vya juu vilivyoinuka.