An-Nisaa
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
إِلَّا ٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلْوِلْدَٰنِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا 98 فَأُو۟لَـٰٓئِكَ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَفُوًّا غَفُورًا 99
{98 - 99} Kisha akawatoa nje wale waliodhoofishwa kwa uhalisia, wale ambao hawana uwezo wa kuhama kwa njia yoyote ile “wala hawawezi kufuata sawasawa njia ya kuhama.” Basi hawa, Mwenyezi Mungu alisema juu yao, “Basi hao, huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kufuta dhambi.” Na “huenda” na mfano wake ni wajibu kutokea kwake kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mujibu wa ukarimu wake na wema wake. Na katika kutaraji thawabu kwa mwenye kufanya baadhi ya matendo, kuna faida, nayo ni kwamba huenda asiyatimize haki ya kuyatimiza, na asiyafanye kwa namna inavyopasa, ambayo inafaa. Bali anaweza kuwa hakuyafanya vyema, kwa hivyo hastahiki thawabu hizo, na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi. Na katika Aya hii tukufu kuna ushahidi kwamba asiyeweza kufanya analoamrishwa miongoni mwa yale ya wajibu na mengineyo, basi yeye amekubaliwa udhuru wake, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema kuhusu wale wasioweza jihadi, “Hakuna lawama juu ya kipofu, wala kiguru hana lawama juu yake, wala mgonjwa hana lawama juu yake.” Na akasema kuhusu ujumla wa maamrisho, “Basi mcheni Mwenyezi Mungu muwezavyo.” Na Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – alisema, “Ninapowamrisha kufanya jambo, basi fanyeni kwalo muwezavyo.” Lakini mtu hapewi udhuru isipokuwa akijitahidi, lakini ikamfungikia milango ya hila, kwa sababu alisema, “wasioweza hila.” Na Aya hii ina tahadharisho kwamba mwelekezi katika Hijja na Umra - na mambo mfano wa mawili hayo yanayohitaji kusafiri - ni katika masharti ya kuwa na uwezo.