An-Nisaa
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَلَا تُؤْتُوا۟ ٱلسُّفَهَآءَ أَمْوَٰلَكُمُ ٱلَّتِى جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمْ قِيَـٰمًا وَٱرْزُقُوهُمْ فِيهَا وَٱكْسُوهُمْ وَقُولُوا۟ لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا 5
Na kauli yake Yeye Mtukufu:
{5} As-Sufaha ni wingi wa safiih, yani asiyekuwa na akili timamu. Naye ni yule asiyeweza kutumia mali yake vizuri: Ima kwa sababu ya kukosa akili, kama vile mwendawazimu, mpumbavu, na mfano wao, au kwa kukosa kwake uamuzi wa busara kama vile mdogo na yule asiyekuwa na uamuzi wa busara. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawakataza walinzi kuwapa watu hawa mali zao kwa kuogopea kuziharibu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alizifanya kuwa ni za kuwakimu waja wake katika masilahi ya dini yao na dunia yao. Na hawa hawawezi kuzisimamia vyema na kuzihifadhi. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawaamuru mlinzi wasiwape mali hizo. Bali awape riziki kutoka humo, na awavishe, na watoe humo yale yanayohusiana na dharura zao na mahitaji yao ya kidini na ya kidunia, na kwamba wawaambie maneno mema. Kwa kuwaahidi wakiomba kuwa watawapa mali hizo baada ya wao kuwa na uwezo wa kufanya uamuzi wa busara na mfano wa hayo. Na wawaongeleshe kwa upole ili kuwatuliza fikira zao. Na katika kufungamanisha kwake Mwenyezi Mungu mali na walinzi, kuna ishara ya kwamba inawalazimu wafanye katika mali za wale wasiokuwa na uamuzi wa busara, kama vile wanavyofanya katika mali zao. Kama vile kuzihifadhi, na kuziendesha, na kutoziachia yenye kuzihatarisha. Na katika Aya hii, kuna ushahidi ya kwamba hela za matumizi za wendawazimu, na watoto wadogo, na wale wasiokuwa na uamuzi wa busara ziko katika mali zao ikiwa wana mali. Kwa kauli yake, "Na walisheni kutoka kwayo, na wavisheni." Na ndani yake kuna ushahidi kwamba maneno ya mlinzi yanakubalika katika yale anayodai kuhusiana na matumizi yanayowezekana na mavazi. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu alimfanya kuwa mdhamini juu ya mali zao. Kwa hivyo, inalazimu kuikubali kauli ya mdhamini.