An-Nisaa
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَقْرَبُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنتُمْ سُكَـٰرَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا۟ مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِى سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا۟ ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰٓ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَآءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ ٱلْغَآئِطِ أَوْ لَـٰمَسْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمْ تَجِدُوا۟ مَآءً فَتَيَمَّمُوا۟ صَعِيدًا طَيِّبًا فَٱمْسَحُوا۟ بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا 43
{43} Yeye Mtukufu anawakataza waja wake Waumini kuikaribia Swala wakiwa wamelewa, mpaka wajue wanayoyasema. Na hili linajumuisha kuzikaribia sehemu za kuswalia, kama vile msikiti. Kwani, hawezeshwi mlevi kuingia humo. Na linajumuisha Swala yenyewe, kwani hairuhusiki kwa mlevi kuswali au kuabudu kwa sababu ya kuchanganyika kwa akili yake, na kutojua kwake yale anayoyasema. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akalipima hilo na akaliwekea kikomo cha kuwepo kwa elimu juu ya yale anayoyasema mlevi. Na Aya hii tukufu ilifutwa kwa kuharamishwa kabisa kwa pombe. Kwa sababu, hapo mwanzo wa Uislamu pombe ilikuwa haijaharamishwa. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawajulisha waja wake uharamu wake kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja kwa kauli yake, “Wanakuuliza juu ya mvinyo na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake.” Kisha Yeye Mtukufu akawakataza mvinyo wakati wa Swala, kama ilivyo katika Aya hii. Kisha Yeye Mtukufu akauharamisha kabisa katika kila wakati kwa kauli yake, “Enyi mlioamini! Hakika, mvinyo, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika matendo ya Shetani. Basi jiepusheni navyo;” hadi mwisho wa Aya. Hata pamoja na haya, uharamu wake unakuwa mkubwa mno wakati wa kuhudhuria Swala; Kwa sababu hilo linajumuisha maharibifu haya makubwa kwa kutofikia lengo la Swala, ambalo ni roho yake na kiini chake, ambalo ni kunyenyekea na uwepo kwa moyo. Kwani mvinyo huulevya moyo na huzuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali. Na inachukuliwa kutoka katika maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja kuzuiwa kuingia katika swala katika hali ya kusinzia kupita kiasi ambapo mwenyewe hahisi anachokisema na anachokifanya. Bali, inaweza kuashiria kwamba anayetaka kuswali akate kila jambo lenye kushughulisha linaloshughulisha fikira yake; kama vile kubana na vile vichafu viwili (haja ndogo na kubwa), na kutaka kukubwa chakula na mengineyo. Kama yalivyokuja hayo katika hadithi sahihi. Kisha akasema, “Wala mkiwa na janaba (msikaribie swala wala msikiti), isipokuwa wanaopita njia (msikitini).” Yani msiikaribie swala katika hali ya mmoja wenu kuwa na janaba isipokuwa katika hali hii, ambayo ni wanaopita njia, yani mnapopitia msikitini bila ya kukaa humo; “mpaka muoge.” Yani mtakapooga ndiyo mwisho wa kumzuia mwenye janaba kuikaribia Swala. Kwa hivyo inaruhusika kwa mwenye janaba kupita tu msikitini. “Na mkiwa wagonjwa, au katika safari, au mmoja wenu akitoka chooni, au mkiwagusa wanawake, na msipate maji, basi ukusudieni.” Basi ikamruhusu mgonjwa kufanya tayammum bila mipaka pamoja na uwepo wa maji au kutokuwepo kwake. Na sababu ya hilo ni ugonjwa ambao ni vigumu kutumia maji. Na vile vile safari; kwa kuwa huwa ni pahali pa uwezekano mkubwa wa kutokuwepo maji. Basi iwapo msafiri atakosa maji, au akipata yale yanayohusiana na mahitaji yake ya kunywa na mengineyo, basi anaruhusiwa kufanya tayammum. Na vile vile ikiwa mtu atapata uchafu kutokana na kukojoa au haja kubwa, au kumgusa mwanamke, basi anaruhusiwa kufanya tayammum ikiwa hakupata maji akiwa nyumbani au safarini, kama linavyoashiriwa hilo na ujumla wa aya hii. Na jumla ya hayo ni kwamba Mwenyezi Mungu aliruhusu kufanya tayammum katika hali mbili: katika hali ya kukosekana kwa maji, na hili halina mipaka, katika hali ya kuwa nyumbani na safarini. Na hali ya pili ni hali ya kupata dhiki kwa sababu ya kuyatumia kwa sababu ya maradhi na mfano wake. Na wafasiri wamehitalifiana katika maana ya kauli yake, "au mkiwagusa wanawake." Je, kilichokusudiwa kwa hilo ni jimai? Ili Aya iwe andiko la moja kwa moja lenye ushahidi wa kuruhusika kufanya tayammum kwa mwenye janaba, kama lilivyokuja hilo kwa wingi katika hadithi sahihi, au kilichokusudiwa kwa hilo ni kugusa tu kwa mkono. Na hilo likafungamanishwa na ikiwa hilo lina uwezekano mkubwa wa kutoka kwa madhii, ambao ni mguso unaotokana na matamanio, ndiyo Aya hii iwe ushahidi juu ya kubatilika kwa wudhuu kwa hilo. Na wanazuoni wa Fiqhi waliitumia kama ushahidi kauli yake, "Na msipate maji" juu ya ulazima wa kuyatafuta maji muda wa Swala unapoingia. Wakasema: 'Kwa sababu haisemekani kuwa hakupata kwa yule ambaye hakutafuta. Bali hilo haliwi hivyo isipokuwa baada ya kutafuta.' Na hilo pia lilitumika kama ushahidi kwamba maji yaliyobadilika kwa kitu miongoni mwa vitu safi yanaruhusika, - bali ni hayo tu yatalazimika kutumiwa katika - kujisafisha kwayo kwa sababu yanaingia katika kauli yake; "Na msipate maji," na haya ni maji. Nao wengine walilipinga hilo kwamba hayo si maji kamili, na kuna maoni tofauti katika hilo. Na katika [aya hii] tukufu kuna uhalali wa hukumu hii kubwa ambayo Mwenyezi Mungu alineemesha kwayo umma huu, ambayo ni uhalali wa tayammum. Na wanazuoni waliafikiana kwa kauli moja juu ya hilo, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu. Na kwamba tayammum inafanywa kwa udongo ambao umeinuka juu ya uso wa ardhi, sawa uwe una vumbi au hapana. Na inawezekana kwamba hilo ni maalum kwa udongo wenye vumbi. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Basi upangusieni kwenye nyuso zenu na mikono yenu;" kutoka kwa huo. Na ule usiokuwa na vumbi haiwezekani kupangusa kwa huo. Na kauli yake, "Basi upangusieni kwenye nyuso zenu na mikono yenu." kutoka kwa huo. Hapa ndipo pahali pa kupangusa katika Tayammum: uso mzima na mikono miwili mpaka kwenye viwiko; kama lilivyoashiriwa hilo na hadithi sahihi. Na inapendekezwa kwamba hilo liwe kwa mpigo mmoja; kama ilivyoashiria hilo hadithi ya 'Ammar. Na ndani yake kuna kwamba Tayammum ya mwenye janaba ni kama Tayammum ya mwingineye katika uso na mikono. Faida: Jua kwamba misingi ya utabibu inazunguka juu ya misingi mitatu: (1) kuhifadhi afya kutokana na vitu vyenye madhara, (2) kuondoa vitu vyenye madhara, (3) kujikinga dhidi yake. Na Yeye Mtukufu alitanabahisha juu yake katika Kitabu chake kitukufu: Ama kulinda afya na kujikinga kutokana na madhara, Yeye Mtukufu aliamrisha kula na kunywa na kutopindukia mipaka katika hilo, na ikamruhusu msafiri na mgonjwa kutofunga saumu ili kuhifadhi afya zao kwa kutumia yale yanayoutengeneza mwili kwa namna ya wastani, na kumkinga mgonjwa kutokana na yenye kumdhuru. Ama kuondoa yenye madhara, Yeye Mtukufu alimruhusu mtu aliye kwenye ihramu ambaye ana vya kumdhuru katika kichwa kwamba anyoe ili kuondoa uchafu unaorundikana ndani yake. Na hili lina tanabahisho juu ya kuondoa kile ambacho ni muhimu zaidi kuliko hayo kama vile mkojo, na kinyesi, na matapishi, na matapiko, na manii, na damu na yasiyokuwa hayo. Alitanabahisha juu ya haya Ibn al-Qayyim, Mwenyezi Mungu amrehemu. Na katika Aya kuna uwajibu kupangusa uso wote na mikono miwili yote, na kwamba inaruhusika kufanya tayammum, hata kama muda haujabaki mfupi, na kwamba haambiwi kutafuta maji mpaka baada ya kuwepo sababu ya wajibu wake. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi. Kisha akahitimisha Aya kwa kauli yake, "Hakika, Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kufuta dhambi." Yani ni Mwingi wa kusamahe na kufuta dhambi kwa waja wake Waumini kwa kurahisisha yale aliyowaamrisha kuyafanya, na kuyasahilisha kwa wepesi wa hali ya juu ili isiwe taabu kwa mja kuyatekeleza na akapata ugumu kwa sababu ya hilo. Na katika msamaha wake na kufuta kwake dhambi ni kwamba aliurehemu umma huu kwa kuweka sheria ya usafi wa udongo badala ya maji wakati haiwezekani kuyatumia. Na katika msamaha wake na kufuta kwake dhambi ni kwamba aliwafungulia wafanyao dhambi mlango wa toba na kurudi kwake, toba na akawaita kwake, na akawaahidi kufutiwa dhambi zao. Na katika msamaha wake na kufuta kwake dhambi ni kwamba Muumini lau kuwa atamjia na madhambi yanayokaribia kujaza ardhi, na akakutana naye hali ya kuwa hamshirikishi na chochote, basi atamjia na kumfutia dhambi kunakokaribia kuijaza.