İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sure 4

An-Nisaa

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 172

لَّن يَسْتَنكِفَ ٱلْمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبْدًا لِّلَّهِ وَلَا ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ ٱلْمُقَرَّبُونَ ۚ وَمَن يَسْتَنكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِۦ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا 172

{172} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kupita kiasi kwa Wakristo kuhusiana na Isa, amani iwe juu yake, na akataja kuwa yeye ni mja wake na Mtume wake. Akataja hapa kwamba yeye hawezi kujiinua juu na kuacha kumwabudu Mola wake Mlezi. "Wala Malaika waliowekwa karibu." Basi akawatakasa kutokana na kujiinua juu ya ibada. Na kuwatakasa kutokana na kiburi ni katika mlango wa linalofaa zaidi. Na kukanusha jambo ndani yake kuna kuthibitisha kinyume chake. Yaani Isa na Malaika waliowekwa karibu wanataka kumwabudu Mola wao Mlezi, na wanaipenda, na wanaifanyia juhudi kulingana na hali zao. Kwa hivyo hilo likawaletea heshima kubwa na kufaulu kukubwa. Na hawakujiinua juu kuwa waja wa umola wake wala uungu wake, bali waliona kulihitajia hilo juu ya kila kuhitaji. Na wala isidhaniwe kwamba kumwinua Isa au asiyekuwa yeye miongoni mwa viumbe ni juu ya daraja lake ambalo Mwenyezi Mungu alimteremsha hapo, na kwamba kuinuka kwake juu ya ibada ni ukamilifu. Bali huo ndio upungufu wenyewe, na ni kitu cha kukashifiwa na kuadhabiwa. Na kwa sababu hii, akasema, "Na mwenye kujiinua juu zaidi ya kumuabudu Yeye Mwenyezi Mungu na akafanya kiburi, basi atawakusanya wote kwake." Yaani, atawakusanya viumbe vyote kwake, wale wanaojiinua juu, na wale wanaotakabari, na waja wake Waumini, kisha atahukumu baina yao kwa hukumu yake ya uadilifu, na malipo yake ya kupambanua.