İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sure 4

An-Nisaa

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 146

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُوا۟ وَأَصْلَحُوا۟ وَٱعْتَصَمُوا۟ بِٱللَّهِ وَأَخْلَصُوا۟ دِينَهُمْ لِلَّهِ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ مَعَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۖ وَسَوْفَ يُؤْتِ ٱللَّهُ ٱلْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا 146

{146} Na hili ni la jumla kwa kila mnafiki, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha kutubia maovu. "Na wakatengenea" katika dhahiri zao na ndani yao. Na wakashikamana naye, na wakamkimbilia katika kuleta manufaa yao na kuwazuia madhara. "Na wakamfanyia peke yake dini yao" ambayo ni Uislamu, na imani, na ihsani "Mwenyezi Mungu." Basi wakaukusudia uso wa Mwenyezi Mungu kwa matendo yao ya dhahiri na ya ndani, na wakajisalimisha kutokana na kujionyesha na unafiki. Kwa hivyo, mwenye kusifika kwa sifa hizi "basi hawa wako pamoja na Waumini." Yani katika dunia hii, na kaburini, na Siku ya Qiyama. "Na Mwenyezi Mungu atawapa Waumini ujira mkubwa." Hakuna ajuaye namna ulivyo isipokuwa Mwenyezi Mungu. Miongoni mwa yale ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio haliwahi kuyasikia, wala hayajawahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote. Na hebu tazama jinsi alivyotaja kushikamana na Yeye na kumfanyia Yeye tu dini kwa namna mahususi, pamoja na kwamba mawili haya yalijumuishwa katika kauli yake; "Na wakatengenea." Kwa sababu kushikamana naye na kumfanyia dini Yeye tu yanaingia katika kutengenea. Na hii ni kwa sababu ya kuhitajika zaidi kwa mawili hayo, hasa katika hali hii ngumu, ambayo unafiki ulikwisha imarika katika mioyo yao, na hauwezi kuondoshwa isipokuwa na kushikamana na Mwenyezi Mungu kwa nguvu na kudumu katika kumkimbilia na kumhitaji katika kuuzuia. Na kwamba kumfanyia Yeye tu kunapingana kabisa na unafiki. Kwa hivyo, kutaja mawili haya ni kwa sababu ya ubora wake, na kusimama kwa matendo ya dhahiri na ndani juu yake, na kwa sababu ya ugumu wa kuyahitaji mawili hayo katika hali hili. Na tafakari vipi ilipotaja kuwa hawa wako pamoja na Waumini, hakusema, "Na atawapa ujira mkubwa" pamoja na kwamba muktadha unawazungumzia wao. Bali alisema, "Na Mwenyezi Mungu atawapa Waumini ujira mkubwa." Kwa sababu, hii kanuni tukufu ni ya jumla ambayo Mwenyezi Mungu hajaacha kuirudia mara kwa mara katika Qur-ani, ikiwa muktadha unajadili baadhi ya mambo madogo. Na Mwenyezi Mungu akataka kwamba kuwe na thawabu au adhabu juu yake, na likawa hilo linaingia katika hayo na masuala mengine madogo yanayoingia ndani yake. Basi analiwekea thawabu kwa kukabiliana na ile hukumu ya jumla ambayo chini yake suala hilo dogo na mengineyo yanaingia, na ili mtu yeyote asifikirie kuwa hukumu hiyo ni mahususi kwa lile suala dogo tu. Na hili ni miongoni mwa siri za ajabu za Qur-ani. Kwa hivyo, mwenye kutubia miongoni mwa wanafiki yuko pamoja na Waumini, na ana malipo yao.