İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sure 4

An-Nisaa

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 116

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِۦ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِٱللَّهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَـٰلًۢا بَعِيدًا 116

{116} Na ahadi hii ya adhabu inayotokana na upinzani huo na kuwahalifu waumini ni daraja mbalimbali ambavyo hawezi kuzihesabu isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee kulingana na hali ya dhambi, iwe ndogo au kubwa. Baadhi yake inamdumisha Motoni na inasababisha kutosaidiwa kabisa. Na baadhi yake ni ya chini ya hivyo. Na pengine aya ya pili ni kama maelezo ya ujumla huu, ambayo ni kwamba ushirikina hausamehewi na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sababu ya kujumuisha kwake kumkashifu Mola Mlezi wa walimwengu wote na [katika] upweke wake. Na kusawazisha kiumbe ambaye haimilikii nafsi yake madhara wala manufaa na Yule ambaye ndiye Mmiliki wa manufaa na madhara, ambaye hakuna neema yoyote isipokuwa ni kutoka kwake anayejitosheleza kikamilifu kwa namna yoyote ile ya kuzingatia. Kwa hivyo, katika dhuluma kubwa zaidi na upotovu wa mbali zaidi ni kutomfanyia Yeye tu ibada kwa Yule ambaye jambo lake ni hivi, na ukuu wake. Na kufanya kitu katika hayo kwa ajili ya kiumbe ambaye hana kitu katika sifa za ukamilifu wala hana kitu katika sifa za kujitosheleza, bali hana isipokuwa kutokuwa na chochote: kutokuwepo, na kutokuwa mkamilifu, na kutojitosheleza, naye ni mhitaji kwa namna zote. Na ama dhambi isiyokuwa ushirikina, miongoni mwa dhambi na maasia, basi hayo yako chini ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akipenda, atamfutia kwa rehema zake na hekima yake, na akitaka, atamwadhibu kwa uadilifu wake na hekima yake. Na Aya hii tukufu imetumiwa kama hoja kwamba Ijmaa ya Ummah huu ni hoja, na kwamba ni imehifadhiwa kutokana na kuwa na kosa. Na sababu yake ni kwamba Mwenyezi Mungu alimuahidi mwenye kuhalifu njia ya Waumini kwamba hatamsaidia, na Moto. Na njia ya Waumini ni neno la umoja lililounganishwa ambalo linajumuisha matendo yote ambayo Waumini wako juu yake miongoni mwa itikadi na matendo. Kwa hivyo watapoafikiana juu ya jambo fulani kuwa ni faradhi, au wakalipendekeza,au kuliharamisha au kulichukia, au kuliruhusu, basi hii ndiyo njia yao. Basi mwenye kuwahalifu katika lolote katika haya baada ya kuafikiana kwao juu yake; basi hakika atakuwa amefuata isiyokuwa njia yao. Na hayo yanaashiriwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Nyinyi mmekuwa bora ya umma waliotolewa kwa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu." Na namna ya kuitumia kama hoja ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alijulisha kwamba Waumini wa Ummah huu hawaamrishi isipokuwa mema. Basi wanapokubaliana juu ya jambo fulani kuwa ni faradhi au wakalipendekeza, basi hilo ni katika yale waliyoamrishwa kuyafanya. Kwa hivyo inabakia tu kulingana na maandishi ya Aya kuwa hilo ni jema, na hakuna kitu baada ya wema isipokuwa maovu. Na vivyo hivyo ikiwa watakubaliana juu ya kukataza kitu, basi hilo ni katika yale waliyokatazwa, basi haliwi isipokuwa ovu. Mfano wa hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu, "Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba umma huu ameufanya Mwenyezi Mungu kuwa umma wa wastani. Yani waadilifu walio bora; ili wawe mashahidi juu ya watu. Yani katika kila kitu; kwa hivyo wakishuhudia juu ya hukumu kwamba Mwenyezi Mungu aliiamrisha, au aliikataza, au aliiruhusu. Basi ushahidi wao umehifadhiwa kwa sababu wanajua kile walichoshuhudia na ni waadilifu katika ushuhuda wao. Na lau kuwa jambo hili lingekuwa kinyume na hivyo,basi hawangekuwa waadilifu katika ushahidi wao wala wenye kuujua. Na Mfano wa hayo ni kauli yake Mola Mtukufu, "Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume." Inaweza kueleweka kutokana na hilo kwamba jambo ambalo hawakuhitilafiana ndani yake. Bali walikubaliana juu yake ni kwamba hawakuamrishwa kulirejesha kwenye Qur-ani na Sunnah, na hilo haliwi isipokuwa lenye kuafikiana na Qur-ani na Sunnah, na haliwi lenye kuhalifu. Basi ushahidi huu na mfano wake unaonyesha kwa mkato kwamba Ijmaa (maafikiano) ya umma huu ni hoja tosha.