İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zumar
Sure 39

Az-Zumar

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 9

أَمَّنْ هُوَ قَـٰنِتٌ ءَانَآءَ ٱلَّيْلِ سَاجِدًا وَقَآئِمًا يَحْذَرُ ٱلْـَٔاخِرَةَ وَيَرْجُوا۟ رَحْمَةَ رَبِّهِۦ ۗ قُلْ هَلْ يَسْتَوِى ٱلَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَٱلَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَـٰبِ 9

{9} Haya ni maneno yanayohusu tofauti iliyopo kati ya yule atendaye mambo ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu na wale wasiofanya hivyo, na baina ya wenye elimu na wasiokuwa na elimu, na kwamba haya ni miongoni mwa mambo ambayo yalishathibiti kwa njia ya yakini katika akili kwamba yanatofautiana. Kwani mwenye kuyapa mgongo mambo ya kumtii Mola wake Mlezi na akafuata matamanio yake, hawi kama mwenye kumnyenyekea kwa kufanya ibada bora kabisa ambayo ni swala, na nyakati bora zaidi ambazo ni nyakati za usiku. Huyu, Mwenyezi Mungu amemuelezea kwa matendo mengi bora zaidi. Kisha akamuelezea kwa hofu na matumaini, na akataja kwamba hofu hiyo inahusiana na adhabu ya Akhera kwa sababu ya madhambi yake yaliyopita, na kwamba matumaini hayo yanahusiana na rehema ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo akamuelezea kwa matendo ya dhahiri na ya ndani. "Sema: 'Ati watakuwa sawa wale wanaojua'" Mola wao Mlezi na wanazijua hukumu zake za kisheria na hukumu zake za kimalipo, siri na hekima alizo nazo katika hayo, "na wale wasiojua" kitu chochote katika hayo? Kamwe hawawi sawa kama vile hauwi usiku na mchana, wala mwangaza na giza, wala maji na moto. "Hakika wanaokumbuka tu ni watu wenye akili" safi, werevu. Hao ndio wanaopendelea cha juu kuliko cha chini. Wanaipendelea elimu kuliko ujinga, na kumtii Mwenyezi Mungu kuliko kumuasi. Kwa sababu wana akili zinazowaelekeza kufikiria matokeo ya mambo. Tofauti na yule ambaye hana akili; yeye anayachukua matamanio yake kuwa ndiyo mungu wake.