İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Furqaan
Sure 25

Al-Furqaan

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

75–76. âyetler

أُو۟لَـٰٓئِكَ يُجْزَوْنَ ٱلْغُرْفَةَ بِمَا صَبَرُوا۟ وَيُلَقَّوْنَ فِيهَا تَحِيَّةً وَسَلَـٰمًا 75 خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۚ حَسُنَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا 76

{75-76} Na ndiyo maana kwa kuwa hima zao na matashi yao yalikuwa ya juu, yakawa malipo yao ni ya aina sawa na matendo yao. Kwa hivyo akawalipa nyumba za juu, ndiyo akasema, "Hao ndio watakaolipwa makao ya juu kwa kuwa walisubiri." Yaani, nyumba za juu na makazi ya kifahari yenye kujumuisha kila kitu kinachotamaniwa na kupendeza macho, na hayo ni kwa sababu ya uvumilivu wao ndio wakapata hayo waliyoyapata, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na Malaika wanawaingilia katika kila mlango. (Wakiwaambia) Assalamu Alaikum (Amani iwe juu yenu), kwa sababu ya mlivyosubiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera." Na ndiyo maana akasema hapa, "na watakuta humo maamkizi na salama" kutoka kwa Mola wao Mlezi, na kutoka kwa malaika wake watukufu, na kutoka kwa wao kwa wao, na watasalimika kutokana na kila yenye kuondoa furaha yao, na kila yenye kuchukiza. Na jumla ya hayo ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwaelezea kwamba wana heshima, utulivu, kujiweka chini mbele yake na mbele ya waja wake, adabu nzuri, ustahamilivu, tabia njema pana, kuwasamahe wajinga na kuwapa mgongo, kukabiliana ubaya wao kwa uzuri, kusimama usiku, kumkusudia Mwenyezi Mungu tu, kuhofu Moto, kumuomba dua Mola wao Mlezi kwa unyenyekevu, kutoka matumizi ya wajibu na yanayopendekezwa, na kuwa wastani katika hayo. Na kama wao ni wastani katika kutoa ambako kwa kawaida mara nyinyi ndani yake kuna kupitiliza kiwango au kufanya chini ya ipasavyo, basi kuwa kwao wastani katika kutoa kwingineko kunafailia zaidi, na kusalimika kutokana na madhambi makubwa, na kusifika na suala la kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika kumuabudu, na kujisafisha mbali na kumwaga damu na kuwaharibia wengine heshima, na kutubia pindi wanapofanya chochote katika hayo, na kwamba hawahudhurii katika vikao vya maovu, na kuvuka mipaka kwa maneno na vitendo, wala wao wenyewe hawayafanyi, na kwamba wanajitenga na upuzi na vitendo viovu, ambavyo havina heri yoyote ndani yake. Na hilo linalazimu kwamba wan uungwana na ubinadamu, na ukamilifu wao na kuziinua nafsi zao dhidi ya kila kauli na kitendo duni, na kwamba wanazikubali aya za Mwenyezi Mungu na kuzifahamu maana zake, na kuzifanyia kazi, na kujitahidi kuzitekeleza hukumu zake, na kwamba wanamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa dua kamili ambayo wanafaidika nayo wao wenyewe, na wanafaidika nayo wote wenye kufungamana nao, na wanafaidika nayo waislamu katika kutengenea kwa wake zao na dhuria wao. Na inalazimu kutokana na hayo kwamba wanafanya bidii ya kuwaelimisha, kuwaaidhi na kuwanasihi. Kwa maana mwenye kukifanyia hima kitu, na akamuomba Mwenyezi Mungu juu yake, hakuna budi wawe wao ndio sababu yake, na kwamba walimuomba Mwenyezi Mungu kuwafikisha daraja za juu iwezekanavyo, ambazo ni daraja za uimamu na ukweli mkubwa. Basi kwa jina la Mwenyezi Mungu, ni za juu namna gani sifa hizi, na ni za juu namna gani hima hizi, na ni makubwa vipi matashi haya, na ni takatifu namna gani nafsi hizi, na ni safi namna gani nyoyo hizi, na hawamwombi Yeye, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kiwango cha juu, na kwamba wanawainua kwa kiwango hiki, na kwamba ni kiwango cha juu iwezekanavyo. Na ni za Mwenyezi Mungu fadhila zilizo juu yao, na neema yake, na rehema zake zilizowafunika, na upole wale ambao uliwafikisha katika nyumba hizi. Na ni za Mwenyezi Mungu neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake kwamba aliwabainishia sifa zao akawaelezea hali zao, akawabainishia hima zao, na akatuwekea wazi malipo yao ili wawe na shauku ya kusifika kwa sifa zao hizo na wafanye juhudi zao katika hilo, na wamuulize yule aliyewaneemesha na kuwakirimu fadhila zake katika kila zama na mahali na kila wakati kwamba awaongoe kama alivyowaongoa, na awasimamie kwa malezi yake maalumu kama alivyowasimamia. Ewe Mwenyezi Mungu, ni zako sifa njema, na kwako ndiko tunakulalamikia, na wewe ndiye unayetegemewa, na wewe ndiye unayeombwa msaada, wala hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwako. Hutuzimilikii nafsi zetu manufaa wala madhara, wala hatuwezi kufanya uzito wa chembe ya heri ikiwa hutaturahisishia kufanya hivyo. Kwa maana, sisi ni dhaifu, hatuwezi kwa kila njia. Tunashuhudia kwamba ikiwa utatukabidhi wenyewe kwa nafsi zetu kwa kiasi cha kupepesa jicho, basi utakuwa umetukabidhi kwa udhaifu, kutoweza, na makosa. Basi hatuna imani ewe Mola wetu Mlezi isipokuwa kwa rehema yako, ambayo kwayo ulituumba, ukaturuzuku, na ukatuneemesha kwa yale uliyotuneemesha ya dhahiri na ya ndani, na ukatuondolea adhabu. Basi turehemu kwamba rehema ambayo kwayo utatutosheleza kutohitaji rehema ya asiyekuwa Wewe. Kwa maana, hawezi kuambulia patupu mwenye kukuomba Wewe na kutumaini.