İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Hajj
Sure 22

Al-Hajj

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

12–13. âyetler

يَدْعُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُۥ وَمَا لَا يَنفَعُهُۥ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلضَّلَـٰلُ ٱلْبَعِيدُ 12 يَدْعُوا۟ لَمَن ضَرُّهُۥٓ أَقْرَبُ مِن نَّفْعِهِۦ ۚ لَبِئْسَ ٱلْمَوْلَىٰ وَلَبِئْسَ ٱلْعَشِيرُ 13

{12 - 13} "Yeye huomba," huyu anaelekea usoni mwake badala ya Mwenyezi Mungu kwa yale ambayo hayamnufaishi wala hayamdhuru, na hii ndiyo sifa ya kila anayeitwa na kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana hana faida wala madhara kwa nafsi yake au kwa ajili ya wengine. "Huko ndiko kupotolea mbali," ambako kumefika mwisho katika mwelekeo; pale anapojiepusha na ́ibaadah ya mwenye kunufaisha, mwenye madhara, tajiri, mwenye kutajirika, na akakubali kuabudiwa kwa kiumbe kama yeye au mdogo kuliko yeye, hana chochote katika udhibiti wake juu ya jambo hilo, bali ni karibu zaidi kufikia kinyume cha makusudio yake. Na ndiyo maana akasema: "Humuomba yule ambaye bila ya shaka dhara yake ipo karibu zaidi kuliko nafuu yake:" kwani madhara yake yamo katika akili, na mwili, na dunia na Akhera ni yenye kujulikana. "Kwa hakika huyo ni mlinzi muovu;" yaani: muabudiwa huyu, "na rafiki muovu." Yaani, rafiki anayeshikamana naye; lengo la Mola ni kupata faida na kuzuia madhara. Ikiwa hakuna chochote kati ya haya kitatokea; ni mwenye kusemwa kwa ubaya na mwenye kulaumiwa.