İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Taa-Haa
Sure 20

Taa-Haa

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 52

قَالَ عِلْمُهَا عِندَ رَبِّى فِى كِتَـٰبٍ ۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّى وَلَا يَنسَى 52

{52} Musa akasema, "Elimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi katika Kitabu. Mola wangu Mlezi hapotei wala hasahau." Yaani, alikwishayadhibiti matendo yao ya heri na maovu, na akayaandika katika kitabu chake, ambacho ni Ubao uliohifadhiwa, na akayazunguka kwa elimu na kuwa na habari zake zote. Kwa hivyo, hapotei kuhusiana na kitu chochote katika hayo wala hasahau yale anayoyajua katika hayo. Na maana yake ni kwamba waliyaendea yale waliyoyafanya na wakayapata matendo yao, na watalipwa juu yake. Basi hakuna faida yoyote katika kuuliza kwako ewe Firauni juu yao. Kwani huo ni umma uliokwisha pita, watapata yale waliyochuma, nanyi mtapata yale mliyoyachuma. Na ikiwa ushahidi tuliokujia nao na ishara tulizokuonyesha uliyahakikisha kwamba ni ya ukweli na ya yakini, na hiyo ndiyo hali yake ya halisi, basi ifuate haki, na uache kufuru, dhuluma na kujadili katika batili kwa wingi. Na ikiwa una shaka nayo, au uliyaona kwamba si yenye unyoofu, basi njia iko wazi, na mlango wa kufanya utafiti haujafungwa. Basi upinge ushahidi kwa ushahidi, na hoja kwa hoja, lakini hutapata njia yoyote ya kufikia hilo maadamu usiku na mchana bado upo (vinapishana). Vipi aweze hilo, na Mwenyezi Mungu tayari alikwisha julisha kumhusu kwamba alizikanusha ishara ingawa alikuwa na yakini nazo? Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na walizikataa kwa dhuluma na kujivuna, na hali ni kuwa nafsi zao zina yakini nazo." Naye Musa alisema, "Wewe unajua bila ya shaka kwamba hakuna aliyeyateremsha haya isipokuwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili yawe ni ushahidi wa kuonekana." Kwa hivyo ikajulikana kwamba alikuwa dhalimu kakita kujadili kwake, ambaye makusudio yake yalikuwa kujiinua katika ardhi.