Al-Baqara
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ ٱلَّذِى ٱسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّآ أَضَآءَتْ مَا حَوْلَهُۥ ذَهَبَ ٱللَّهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِى ظُلُمَـٰتٍ لَّا يُبْصِرُونَ 17
(17) Yani mfano wao unaoingiana na walivyo ni mfano wa yule aliyewasha moto, yani alikuwa katika giza kubwa na akihitaji moto vikubwa. Basi akauwasha kutoka kwa mtu mwingine, na haukuwa tayari pamoja naye, bali alichukua kutoka kwa mwingineye. Pindi moto ulipoangaza vilivyokuwa kandokando yake, na akatazama mahali ambapo yeye yupo na hofu iliyopo hapo, na amani yake (moto huo), na akanufaika na moto huo, na macho yake yakaburudika kwa moto huo; na akadhani kuwa ana uwezo juu yake. Basi, alipokuwa hivyo, hapo Mwenyezi Mungu akaiondoa nuru yake, kwa hivyo, nuru hiyo ikamtoka na furaha ikaondoka pamoja nao, na akabaki ndani ya giza totoro na moto wenye kuchoma. Kwa hivyo, kule kuangaza kulikokuwa ndani yake kukaondoka, na kukabaki kule kuchoma kuliomo ndani yake, basi akabaki katika giza mbalimbali: giza la usiku, giza la mawingu, giza la mvua na giza lilichotokea baada ya nuru hiyo. Basi inakuaje hali ya huyu anayeelezwa? Kadhalika, wanaafiki hawa waliwasha moto wa imani kutoka kwa Waumini, na haikuwa sifa yao. Basi wakapata mwangaza wake kwa muda, na wakanufaika. Kwa hivyo, damu zao zikahifadhika kwa hilo, na mali zao zikasalia salama, na wakapata usalama fulani katika dunia hii. Na walipokuwa hivyo, mauti yakawashambulia ghafla na yakawanyang'anya kunufaika na nuru hiyo, na wakapatwa na kila wasiwasi na dhiki na adhabu. Na wakapatwa na giza la kaburini, na giza la ukafiri, na giza la unafiki, na giza la maasia kwa aina zake mbalimbali. Na baada ya hayo, giza la Moto, na ni makazi mabaya mno. Ndio maana Mwenyezi Mungu alisema kuwahusu: