İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Kahf
Sure 18

Al-Kahf

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 19

وَكَذَٰلِكَ بَعَثْنَـٰهُمْ لِيَتَسَآءَلُوا۟ بَيْنَهُمْ ۚ قَالَ قَآئِلٌ مِّنْهُمْ كَمْ لَبِثْتُمْ ۖ قَالُوا۟ لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۚ قَالُوا۟ رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثْتُمْ فَٱبْعَثُوٓا۟ أَحَدَكُم بِوَرِقِكُمْ هَـٰذِهِۦٓ إِلَى ٱلْمَدِينَةِ فَلْيَنظُرْ أَيُّهَآ أَزْكَىٰ طَعَامًا فَلْيَأْتِكُم بِرِزْقٍ مِّنْهُ وَلْيَتَلَطَّفْ وَلَا يُشْعِرَنَّ بِكُمْ أَحَدًا 19

{19} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, "Na kwa namna hiyo tuliwainua usingizini" mwao mrefu, "ili wapate kuulizana wao kwa wao" na wapate kujua uhakika wa kipindi walichokaa hapo. "Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku." Hili linatokana na dhana ya mzungumzaji huyo. Na ni kana kwamba walichanganyikiwa kuhusiana na urefu wa muda huo. Na ndiyo maana, "wakasema: Mola wenu Mlezi ndiye anayejua zaidi muda mliokaa." Kwa hivyo, wakarudisha elimu kwa Yule aliyezunguka kwa elimu yake kila kitu kwa ujumla na undani. Na huenda Mwenyezi Mungu Mtukufu baada ya hayo aliwajulisha muda wa kukaa kwao hapo. Kwa sababu aliwainua usingizini ili waulizane wao kwa wao, naye akatoa taarifa kwamba waliuliza na kusema kulingana na waliyokuwa nayo, na jambo lao la mwisho likawa shaka. Lazima aliwaambia kwa uhakika. Tunayajua haya kutokana na hekima yake katika kuwatuma, na kwamba hafanyi hivyo bure, na kutoka kwa rehema yake kwa wale wanaotafuta elimu ya ukweli katika mambo yanayotakiwa kujulikana na kujitahidi kufanya hivyo kadiri inavyowezekana. Mwenyezi Mungu anambainishia hilo, na katika yale aliyoyataja baadaye katika kauli yake: “Na namna hivi ndivyo tulivyowajulisha kwa watu wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa (Qiyama) haina shaka.” Lau asingepata elimu ya hali yao, isingekuwa ushahidi wa kile kilichotajwa.